BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limewafukuza kazi watumishi wake wanne, kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya utoro kazini na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya shilingi milioni 46,680,000.
Waliofukuzwa kazi ni Mosta Ndunguru ambaye ni Afisa tabibu na Bapara Mwang’ombe Mhudumu wa afya ambapo wote kwa pamoja wamefukuzwa kwa makosa ya utoro kazini. Walioisababishia hasara halmashauri hiyo ya shilingi milioni 46,680,000 ni maofisa misitu wasaidizi, Kelvin Haulle na Ally Almasi. Msikilize mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ambrose Nchimbi
0 Comments