
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Kanyatta
akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi
kunavyoathiri sekta ya utalii katika semina iliyofanyika jana mjini
Dodoma .

Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Yussuf Hussein,
akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu utalii wa baharini ambao
umekuwa haupewi kipaumbele katika kutangazwa pamoja na kuendelezwa
katika semina hiyo.

Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Marwa Chacha,
(katikati) akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na
wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu wanyamapori
waharibifu wa mazao kama vile tembo wanavyoathiri maisha ya wapiga kura
wake kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika
semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo
.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye,
(katikati) Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (
kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo
Makani ( wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa makini michango ya wajumbe
wa kamati hiyo wakati walipokuwa wkichangia hoja kuhusu mada mbalimbali
zilizotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu
madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa
tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa
mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini,
iliyofanyika jana mjini Dodoma.

Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Devota Minja, MB (
wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia
kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa
Wizara hiyo kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi,
tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na
wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka
hifadhi nchini katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Kwa upande
wa kushoto ni viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii .

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi ( wa
kwanza kulia) pamoja na na viongozi wa taasisi katika semina ya
kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii iliyofanyika jana mjini
Dodoma .
0 Comments