Beki
kisiki wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris jana jioni alianza rasmi
mazoezi mepesi ya kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya mabingwa
watetezi, Yanga.
Hiyo,
ikiwa ni siku moja tangu washambuliaji wa Yanga Mzimbabwe, Donald Ngoma
na Mrundi, Amissi Tambwe wapone majeraha ya goti na kuanza mazoezi ya
kujiandaa na mchezo huo.
Timu
hizo, zinatarajiwa kuvaana Aprili Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani
mkubwa.
Morris
alisema anarejea uwanjani baada ya kupata nafuu ya majeraha yake ya
mfupa wa paja la kulia wakati timu hiyo ilipocheza mchezo wake wa Kombe
la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland.
“Namshukuru
Mungu kwa kuweza kurejea uwanjani kwa sababu mchezaji lengo lake ni
kucheza na siyo kukaa tu, hamna kitu kibaya kwa mchezaji kama kupata
majeraha yatakayosababisha kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
“Hivyo,
hivi sasa nimepata nafuu ya majeraha yangu na kuanza mazoezi mepesi ya
binafsi kabla ya kuanza programu ya mazoezi magumu na wenzangu katika
kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga,” alisema Morris.

0 Comments