Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Geita haikuwa nyumba katika shughuli hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akikagua na kuangalia namna ambavyo shamba hilo limelimwa.
Mkuu
wa wilaya ya Geita,akiteta jambo na baadhi ya wananchi na mwenyekiti wa
mtaa pamoja na diwani wa kata ya Mtakuja kabla ya zoezi la kuondoa zao
hilo.
Shughuli
ya uondoaji wa Bangi ikiendelea Mkurugenzi wa Mji wa Geita ambaye
amevaa Mkoti wa suti Mhandisi Modest Aporinaly akigoa moja kati ya mmea
wa Bangi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita,Ali Kidwaka akishughulika.
Mwandishi wa Habari wa Storm Fm,na Mmiliki wa mtandao wa Maduka Online Joel Maduka akiendelea na majukumu.
Ulinzi ukiwa umeimalishwa.
Bangi ambayo ilikuwa imekwisha kukomaa kwaajili ya kuuzwa ikioneshwa kwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.
Zoezi la kuchoma likiendelea.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
PICHA NA JOEL MADUKA
Mkuu
wa wilaya ya Geita Herman Kapufi ameteketeza na kuvuruga shamba la
Bangi ambalo linasadikika kuwa na ukubwa wa hekari mbili na nusu la
Bangi huku akisisitiza kuwa hakuna mtu yoyote atakeyepona ndani ya
Wilaya yake iwapo atabainika anajihusisha na madawa ya kulevya ambayo
yamekuwa ni hatari kwa vijana wengi.
Mkuu
huyo wa Wilaya alitoa kauli hiyo jana wakati wa zoezi la
kuteketeza kwa moto mimea ya bangi kwenye shamba ambalo lipo Mtaa wa
Samina B kata ya Mtakuja iliyopo halmashauri ya Mji wa Geita.
Kapufi
alisema vijana wengi wanaokaa kwenye vijiwe wanaangamia kwa uvutaji wa
bangi na kwamba watu wanaojishughulisha na ulimaji pamoja na usambazaji
hatasita kuwachulia hatua kali za kisheria, huku akitoa rai kwa
wananchi kuwafichua wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.
‘’Ndani
ya Wilaya yangu sitasita kuwachulia hatua watu wote wanaojihusisha na
ulimaji ikiwemo usambazaji wa madawa ya kulevya hatuwezi kuona vijana
ambao ni nguvu kazi ya taifa wakiteketea kwa madawa hatutakubali…lakini
niwashukuru wananchi waliotupatia taarifa kuwepo kwa shamba hili ambalo
leo [jana] tunachoma motomimea ya bangi’’alisema Kapufi.
kwa
upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa samina B. John Balenge
alisema kuwa walipata taarifa za shamba hilo la bangi kutoka kwa
wananchi waliokuwa wakienda porini kufanya shughuli za kutafuta kuni na
mkaa na kwamba waliweka mtego wa kumnasa mwenye shamba bila mafanikio.
‘’Ndugu
waandishi kama mnavyoona shamba hili linaonesha mwenye nalo alikuwa
akilitunza limesafishwa vizuri niseme tu sisi tulipata taarifa kwa
wananchi tukawa tunaweka ulinzi wa kumkamata mmiliki ni mwezi sasa bila
mafanikio,’’alisema mwenyekiti huyo.
Naye
diwani wa kata ya Mtakuja ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa
halmashauri ya Mji wa geita Constatine Morand alisema hayuko tayari
kumuona mtu akifanya biashara ya madawa ya kulevya katika kata yake na
kwamba wanamuunga mkono rais katika vita hiyo.
‘’Nitowe
wito kwa wananchi wote wa kata ya Mtakuja siko tayari kuona biashara
hii ikiendelea kwenye kata yanngu na kuangamiza watanzania wengi…na sisi
huku chini tunamuunga mkono rais wetu Dk. John Magufuli katika vita hii
waliyoianzisha,’’alisema morandi.
Akizungumza
na MADUKA ONLINE mmoja katti ya vijana ambao walikuwa wakitumia Bangi
hapo zamani na kuamua kuachana nazo ,Juma Suleiman alisema madawa hayo
ya kulevya hayana faida yoyote na badala yake yanatia hasara kwa vijana
na kurudisha maendeleo nyuma.
Kutokana
na biashara hii ya bangi kushamiri katika visiwa vilivyoko mwambao wa
ziwa victoria, Mkuu wa Wilaya alisema wakimaliza oparesheni maeneo ya
nchi kavu watahamishia nguvu majini kwenda kupambana na wafanyabiashara
wa zaohilo haramu.
No comments:
Post a Comment