Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa tawi hilo la Benki ya ABC Tegeta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya ABC, Dana Botha akizungumza jambo katika hafla hiyo
…Mpango akisaini katika kitabu cha wageni alipofika kwenye tawi hilo.
Meza kuu ilivyoonekana katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa wateja binafsi wafanyabiashara wadogo na kati, Joyce Molai akifafanua jambo katika hafla hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba yake.
Waziri Mpango akifunguliwa akaunti ya ABC baada ya uzinduzi kukamilika.
Wafanyakazi wa benki ya ABC Tawi la Tegeta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mpango.
Mpango akiagana na viongozi hao.
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango amesema kuwa anafurahishwa na
huduma za kifedha hasa za mabenki zinapowafuata wananchi nje ya miji na
kupata huduma mbalimbali bila kuhangaika kufika mjini.
Hayo ameyasema leo wakati akifungua Tawi la Benki ya ABC lililopo Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo alisema kuwa : “Namshukuru Mwenyekiti wa Bodi,
Wajumbe wa Bodi, Uongozi wa Benki ya ABC kwa kunialika kufungua tawi
hili la Tegeta. Mimi kama waziri wa fedha napata faraja ninapoona huduma
za fedha zinakua na hasa zinapowafuata wananchi walio nje ya miji.”
Alielezea
kuwa anaushukuru uongozi wote wa benki hiyo kwa kupanua huduma hiyo ili
kuwafikia wananchi wengi zaidi hadi kuwafikia wananchi walio wengi
vijijini.
“Serikali
ingependa kuona huduma za taasisi za fedha zikielekezwa zaidi kwenye
vijiji vya wilaya pembezoni ambako kuna Watanzania wengi ambao nao
wanahitaji kupatiwa huduma za kibenki.”
Aidha
aliwaomba uongozi mzima wa Benki ya ABC kufikisha zaidi huduma yao
pembezoni mwa miji na kupata huduma za kibenki bila vikwazo na masharti
magumu.
“Ni
matarajio ya wengi kuwa kufunguliwa kwa tawi hili hapa Tegeta kutakata
kiu ya wajasiriamali waliokuwa wakisubiri kwa hamu kupata mikopo kwani
itawasaidia kuinua hali zao za maisha na pia kuchangia pato la taifa kwa
kushirikiana katika uzalishaji mali kutokana na shughuli mbalimbali
wanazofanya.
Naye
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na Kati, Joyce
Molai aliwaomba wananchi kujitokeza katika Benki ya ABC hasa Tawi la
Tegeta ili kuweza kujionea huduma wanazozitoa na kufungua akaunti za
kutunza amana zao, na wateja wao kupata fursa ya kuomba mikopo nafuu ya
kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi.









0 Comments