| ||
![]() |
Picha mbalimbali za waigizaji filamu, wanamuziki pamoja na wadau
wengine wa filamu waliohudhuri katika uzinduzi wa filamu ya Kiumeni
katika ukumbi wa filamu wa Mlimani City.
Picha na Emmanuel Massaka
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
FILAMU ya Kiumeni iliyogizwa na Ernest Napoleon, Idris Sultan pamoja na Antu Mandoza imeingizwa rasmi sokoni jana na itaanza kuoneshwa katika Ukumbi wa Mlimani City.
Katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na waigizaji mbalimbali wa filamu, wanamuziki pamoja na wadau wengine katika ukumbi huo.
Mwigizaji Ernest aliwahi kutamba katika filamu ya Going Bongo, katika filamu ya Kiumeni ameigiza kama kijana ambae ametokea maisha ya watu wenye uchumi wa kifedha na kisha kuwa na uhusiano na msichana Antu ambae ametokea kwenye familia ya maisha ya familia ya kipato kidogo.
Katika filam hiyo , Ernest anaenda kujitambulisha katika familia ya Antu ambapo anachukua gari jipya la baba yake aina ya Noah anamdanganya kuwa anaenda kumwekea system nzuri ya muziki, ambapo mzazi wake huyo anamsihi alitunze bila ya kujua kuwa mwanawe anaenda nalo uswahilini kujitambulisha.
Alipofikia maeneo ya nyumbani kwa akina Antu aliliegesha mtaani na saa chache baadae lilibiwa kila kitu na ndipo mchakato wa kuwatafuta wezi ulipoanza na akajikuta anakuja kuangukia mikononi mwa Idris ambae ndio kinara wa uhalifu katika eneo hilo na alikuwa ana uhusiano na Antu miaka ya nyuma.
filamu ya kiumeni ina mfululizo wa matukio kadhaa ambayo yanachekesha na kufundisha, lakini pia katika filamu hiyo kuna ushabiki wa Yanga na Simba na pia yupo Rashid Matumla.
Tiketi za kuangalia filamu hiyo zimeshaanza kuuzwa ambapo inaanza kuoneshwa rasmi kesho katika Ukumbi Cinema Century wa Mlimani City.






0 Comments