Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akitoa nasaa kwa
wanawake na vijana walioathirika na janga la madawa ya kulevya kituoni hapo
mapema leo asubuhi.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akimpa mkono wa
pongezi mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe kwa jitihada anazoendelea
kuzifanya katika kuhakikisha waathirika wote wa madawa ya kulevya waliopo
kituoni kwake wanapata elimu ya kutosha na hatimaye kuacha kabisa utumiaji wa
madawa hayo.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika
ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa
madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko
kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni
Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji.
Moja
ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi. Jacqueline
Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada
waliowapatia.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi (kushoto)
akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa kituo
People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef), Nuru Salehe wakati wa sherehe ya maadhimisho
ya siku ya wanawake Duniani mapema leo asubuhi. Kulia ni Jacqueline Samson na
Ashura Diwani.
Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation
(Pedderef) bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya
pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo,
ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya
kupewa elimu na malezi yanayostahili.
.............................
Katika kuadhimisha siku
ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani
kuadhimisha siku hiyo
Mrakibu Msaidizi wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo
Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano
(5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi
aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na
kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.
Ambapo aliiomba jamii
isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii
kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili
wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na
kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.
Pia Nzalayaimisi
aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote
waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga
hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza
mapambano hayo.
Mkurugenzi wa kituo
hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba
taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani
wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni
hapo.






0 Comments