Mtambo wa kudhibiti vumbi katika kiwanda cha
saruji cha Moshi ambao haufanyi kazi ipasavyo, kumekua na malalamiko kutoka kwa
wananchi juu ya uchavuzi wa hewa ufanywao na kiwanda hicho. Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Kaskazini ilitoa maelekezo
ambayo hayakutekelezwa kikamilifu, hivyo
kiwanda hicho kimefungwa hii leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba alipotembelea kiwanda cha saruji cha Moshi.
Kiwanda hicho kimefungiwa baada ya kutotekeleza maagizo waliyopewa na Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Katikati ni Mwakilishi wa Kiwanda
hicho Bi. Sophia na kushoto ni Dkt. Menan Jangu kutoka Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kaskazini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi.
Agness Hokororo mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ziara ya kikazi.
Na
Lulu Mussa Moshi
Ziara
ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba hii leo ametembelea Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Rombo. Akiwa
Wilayani hapo Waziri Makamba ametembelea Kiwanda cha Saruji cha Moshi kufuatia
malalamiko ya wananchi juu ya uchafuzi wa hewa itokanayo na vumbi katika
shughuli za uzalishaji.
Akitoa
maelezo wa awali, Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo amesema kuwa
Kiwanda hicho kimeendesha shughuli za uzalishaji wa sementi kwa kutofuata
sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mfumo mzuri wa
kudhibiti uchafuzi wa vumbi kiwandani hapo.
kwa
upande mwingine Dkt. Menan Jangu Mratibu wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kaskazini amesema kuwa
Ofisi yake awali ilitembelea kiwanda hicho na kutoa muongozo na taratibu
zinazotokiwa kufuatwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
"Tuliwaelekeza
kufanya yafuatayo, kujenga fensi kuzunguka eneo lote la kiwanda, kujenga
"pevements" na kuweka mashine maalumu ya kuzuia vumbi kusambaa kwa
wingi angani, vitu ambavyo havijafanyiwa kazi." Alisisitiza Dkt. Jangu
Mwakilishi
wa Kiwanda hicho raia wa China aliyefahamika kwa jina moja tu Bi. Sophia,
amesema kuwa suala la kuzungusha uzio eneo lote litatekelezwa pindi hati miliki
ya ardhi ya eneo hilo itakapopatikana.
Waziri
Makamba aliagiza NEMC kukifunga kiwanda hicho mpaka mapendekezo yaliyotolewa na
Baraza yatakapokamilika. "Kiwanda hiki kisitishe shughuli za uzalishaji
mpaka pale vigezo vya Sheria ya Mazingira vitakapokamili"
Katika
hatua nyingine Waziri Makamba ametembelea Ziwa Chala na kuwataka wadau wa
mazingira kuongeza jitihada katika kulihifadhi
kwa kuwa ni muhimu kwa ikolojia na historia yake. " Kina cha ziwa
hili kinashuka kwa kasi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na sisi
kama Serikali tutahakikisha tunawekeza nguvu zetu katika kunusuru kina cha ziwa
hili kisiendelee kushuka" Alisisitiza Makamba.
Waziri
Makamba ameahidi kuzungumza na Serikali ya Kenya ili kuwa na mikakati ya pamoja
ya kuhifadhi ziwa hilo kwa kukuwa lipo pande zote za nchi hizi. Ziwa Chala ni
chanzo kikubwa cha utalii na limetokana na mlipuko wa Volcano likiwa halitoi
wala kuingiza maji kutoka vyanzo mbalimbali.
Waziri
Makamba amemaliza ziara yake Mkoani Kilimanjaro na hii leo amewasili Mkoani
Arusha.



0 Comments