Mshindi wa Divisheni A Nett Mashindano ya Enntebe Ladies
Open 2017 kutoka Klabu ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika harakati ya Mchezo
huo katika Michuano iliyofanyika Uganda Hivi Karibuni.
Mshindi wa Divisheni A Nett Mashindano ya Enntebe Ladies
Open 2017 kutoka Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya
Lugalo Vicky Elias akiwa katika harakati ya Mchezo huo katika Michuano
iliyofanyika Uganda Hivi Karibuni.
Bingwa Mashindano ya
Wachezaji wa Ridhaa ya Moshi Mwaka 2016 Nicholous Chitanda akiwa katika
harakati za mchezo huo.
( Picha na Luteni Selemani Semunyu)
....................
Na Luteni Selemani
Semunyu JWTZ
Klabu ya Gofu ya jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya
Lugalo imejivunia kuanza vyema mwaka 2017 baada ya Mchezaji wake Vicky Elias kuibuka na ushindi wa Divisheni A Nett katika Mashindano ya
Wanawake Enntebe Ladies Open yaliyomalizika
hivi Karibuni nchini Uganda.
AKizungumza na Waandishi wa habari mwenyekiti wa Klabu hiyo
Brigedia Jenerali Mstaafu Michael
Luwongo alisema Ushindi huo ni ishara tosha ya Mafamikio ya Kimchezo kwa mwaka
2017 kwani alikuwa mtanzania pekee kati ya Wachezaji 53 walioshiriki.
" Unajua tunajipanga kimataifa na tuliahidi kuweka
nguvu katik mashindano kimataifa ,kwa mwaka 2017 na huu ndio mwanzo hivyo
mashabiki wa Lugalo na Wanachama wajipange kufuarahia Timu yao kutokana na
mafanikio yatakayopatikana kimataifa.
Aliongeza kuwa licha ya matokeo ya Kimataifa pia Michezo yeyote
ambayo Timu ya Gofu ya Lugalo itaalikwa
basi watahakikisha wanafanya vyema ili adhama ya Timu ya Gofu ya Lugalo kuwa
Timu Bora inatimia.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa ushindi wa Vicky ni Ushindi
Mkubwa kutokana na Maandalizi pamoja na Washiriki waliojitokeza kushiriki
michuano hiyo lakini ni sifa kwa Nchi kw sababu mbali na kutoka Klabu ya Lugalo
lakini kubwa zaidi ni Mtanzania.
Kwa Upande wake Vicky Elias alisema mashindano yalikuwa
magumu lakini alipambana kufa na kupona kurejesha heshima ya Klabu na Nchi kwa
Ujumla na kufanikiwa kurejea na ushindi ambao haikuwa rahisi kwani siku ya
kwanza alipiga mikwaju 83 na kutoa kiwango chake cha uchezaji ambacho ni Tisa.
Katika siku ya pili ya mashindano hayo Vicky aliibuka na Mikwaju
ya Jumla 81 baada ya kutoa kiwango chake cha Uchezaji cha Tisa na hivyo kuibuka na Ushindi wa
Kwanza Divisheni A na kuwashinda
Wachezaji Wenzake kutoka Uganda na Kenya waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Wakati huo huo
kufuatia Maandalizi ya mashindano ya wachezaji wa Ridhaa nchini Tanzania
Amature Stoke Play yanayotarajiwa kufanyika Moshi mkoani Kilimanjaro machi
12 Wachezaji wa Timu ya Lugalo
wanaendelea na Mazoezi kujiwinda na Michuano hiyo.
Bingwa mtetezi wa mashindano ya hayo kutoka Lugalo Nicholous Chitanda amesema yuko katika
maandalizi kujiandaa na michuano hiyo ili kutetea Ubingwa wake alionyakua mwaka
jana ili kuhakikisha unabaki katika Klabu ya Lugalo.



0 Comments