Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Idara ya
Uhamiaji Zanzibar, wakati wa ziara ya kukagua udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya
Visiwani humo, huku akiagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana
kudhibiti madawa hayo ambayo yanaharibu nguvu kazi ya Taifa.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna wa Jeshi la
Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, akitoa taarifa za utekelezaji wa zoezi la
kudhibiti Dawa za Kulevya Visiwani humo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa ziara ya naibu waziri
kufuatilia utekelezaji wa zoezi la kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya
Visiwani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha, akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni
(wakwanza kushoto), juu ya hatua zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji na vyombo
vingine vya Ulinzi na Usalama kukabiliana na udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya
kiwanjani hapo.Wapili kushoto ni Naibu
Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisikiliza jinsi mifumo ya kudhibiti uingiaji haramu inavyofanya
kazi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha.Ziara
ya Naibu Waziri huyo ilikua na lengo la kukagua mifumo inayotumika kudhibiti
uingiaji wa Dawa za Kulevya.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akitoa maelezo kwa watumishi wa
Idara ya uhamiaji waliopo Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya
Visiwani Zanzibar.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiteta jambo na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum
wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya
katika Uwanja wa Ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.






0 Comments