Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauniakizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi pamoja na Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya
Wizara yake mkoani humo. Katika
mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuanzisha Kituo
cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu pamoja maandilizi ya
Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi
Wilaya ya Ruangwa, Joseph Kiyengialipokuwa anatoa taarifa yake katika Kikao cha
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa ambacho
kilijumuisha Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya Wizara hiyo mkoani Lindi. Katika mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji kuanzisha Kituo cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi
Aprili mwaka huu pamoja maandilizi ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani
humo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauniakimpa maelekezo Fundi Mkuu wa ujenzi wa Gereza Ruangwa
(kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo
unaoendelea mjini Ruangwa. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi,
Tusekile Mwaisabila.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya
Ruangwa, Joseph Kiyengi wakati alipokuwa akionyesha eneo litakalojengwa Kituo
kipya cha Polisi wilayani humo. Maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho
yameshaanza. Katika ziara yake Masauni pia aliagiza uanzishwaji wa Kituo cha
Zimamoto wilayani humo haraka iwezekanavyo. Katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya
hiyo, Twaha Mpembenwe.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
.....................................................
NAIBU Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
kuanzisha kituo cha zimamoto Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Masauni alisema Aprili Mosi mwaka huu
Jeshi hilo litakuwa na ofisi wilayani humo ili askari wa Jeshi hilo waanze
kutoa huduma sehemu mbalimbali ya Wilaya hiyo ambayo ni muhimu kituo hicho
kuwepo kutokana na uwepo na machimbo ya madini ya dhahabu pamoja na mji kuendelea
kukua kwa kasi.
“Tumekubaliana vizuri baada ya Kamanda
wa Zimamoto mkoa kuwa ifikapo tarehe moja askari wa zimamoto watakuwepo hapa
Ruangwa rasmi kwa ajili ya kuanza kazi, na watapewa ofisi na halmashauri ya
Wilaya, hivyo utaratibu wa kupata vifaa vya awali uanze mara moja kama
tulivyokubaliana,” alisema Masauni.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi hilo
Mkoa wa Lindi, Christina Sunga alimuhakikishia Naibu Waziri pamoja na Watendaji
wa Wilaya hiyo, agizo hilo atalifanyia kazi haraka iwezekanavyo na mpaka
ifikapo Aprili mosi mwaka huu tayari askari wawili watakuwa wameripoti mjini
Ruangwa.
“Uwepo wa askari hawa kutarahisisha kwa
kiasi kikubwa kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuzima moto pamoja na kupambana na
uzimaji moto, licha ya kuwa tunakuwa na vifaa vya awali vya uzimaji moto mpaka
hapo tutakapopata gari kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uzimaji moto na
utoaji elimu zaidi,” alisema Sunga na kuongeza;
“Tunashukuru Halmashauri ya Wilaya ya
Ruangwa kwa kutupa ofisi kwa ajili ya askari wa zimamoto lakini pia kutuwezesha
kupata vifaa hivyo vya awali vya uzimaji wa moto.”
Aidha, Masauni alimuagiza Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Lindi, (RPC) Renatha Mzinga kuandaa mchoro pamoja na gharama ya
ujenzi wa kituo kikubwa cha polisi cha Wilaya ya Ruangwa ili ujenzi huo uanze.
“Nimekagua eneo la ujenzi wa kituo kipya
cha polisi, eneo zuri na linafaa kwa ujenzi wa kituo kikubwa cha polisi,
maandalizi tayari yameanza na hivi karibuni RPC atakamilisha mchoro pamoja na
gharama ya ujenzi wa kituo hicho hapa Ruangwa,” alisema Masauni.
Pia Masauni amesema Wizara yake itahakikisha
inawajengea ofisi Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) pamoja na
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani humo ambapo kwasasa ofisi hizo zipo
katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Naibu WaziriMasauni amemaliza ziara yake
ya siku mbili kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na
kuzungumza na askari na maafisa wa vyombo walio chini ya wizara yake mkoani
Lindi na tayari amesafiri mkoani Mtwara kuendelea na ziara yake.




0 Comments