Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (katikati), akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha
Mzinga (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anakagua Makazi ya askari Polisi,
Mitwero mkoani humo ambapo nyumba za askari hao zimechangaa na chache kutokana
na wingi wa askari hao. Hata hivyo, Serikali hivi karibuni inatarajia kujenga
nyumba mpya katika eneo hilo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga
akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
eneola Mitwero mkoani humo ambalo nyumba za makazi ya askari polisi zitakapojengwa.
Masauni alikagua nyumba wanazoishi askari hao kwasasa pamoja na kukagua eneo
hilo makazi mapya yatakapojengwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (katikati), akilikagua Jengo jipya la ghorofa la Idara ya
Uhamiaji Mkoa wa Lindi ambalo linajengwa mjini humo. Kulia ni Afisa Uhamiaji
mkoa huo, George Kombe, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
Masauni aliongozana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya
Wizara yake mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia), akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,
Renatha Mzinga (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anaangalia
ramani ya ujenzi wa makazi ya askari polisi eneo la Mitwero mkoani humo.
Masauni yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kulia)
akimkaribishaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ofisini
kwake kwa ajili ya kupewa taarifa ya mkoa huo, wakati Naibu Waziri Masauni
alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa na Askari wa vyombo vya Ulinzi na
Usalama vilivyo chini ya Wizara yake, katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza, mjini
Kilwa mkoani Lindi. Masauni aliwataka maafisa na askari hao kuongeza nguvu
zaidi katika ukamataji wa wahamiaji haramu pamoja na wauza dawa za kulevya.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.






0 Comments