Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kilambo kilichopo
mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Masauni aliwataka wananchi hao kudumisha
amani mpakani hapo pamoja na kufuata sheria za uhamiaji za nchini pamoja na za
Uhamiaji Msumbiji endapo watahitaji kuvuka mpaka huo. Masauni baada ya kukagua
mpaka huo aliwataka maafisa wakekuimairisha ulinzi zaidi mpakani hapo. Wapili
kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake kukagua mpaka wa Tanzania na
Msumbiji uliopo katika Kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara, Evod Mmanda. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama,
na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kushoto) akiwapa maelekezo maafisa wake wakati alipokuwa Mto Ruvuma,
Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara.Wapili
kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na anayefuata ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza
Mkoa wa Mtwara, Ismail Mlawa kwa ajili ya kwenda kukagua nyumba za askari
Magereza wa Gereza Lilungumkoani humo ambazo zinahitaji marekebisho kutokana na
kuharibika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata
Gesi Asilia Madimba wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), mkoani
Mtwara, Mhandisi Sultan Pwaga, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara
kiwandani hapo kuangalia jinsi gesi inavyozalishwa. Hata hivyo, Masauni alitoa ahadi, Jeshi lake litafanya
taratibu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda (katikati)
pamoja na TPDC kufanikisha uwepo wa Kituo cha Polisi kama walivyoomba uongozi
wa Kiwanda hicho kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kiwandani hapo pamoja na
wananchi waishio jirani na kiwanda hicho.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.





0 Comments