Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mtu moja
ambaye jina lake hajijafahamika ameuawa na wananchi wenye hasira
kali huko maeneo ya kwa Mrombo Jijini Arusha ,akidhaniwa kuwa ni mwizi
wa pikipiki baada ya mtu huyo kupita na kufananishwa na waendesha
pikipiki hao.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo ambapo amesema kuwa majira ya saa saba mchana
wananchi hao walimuona mtu huyo wakadania kuwa ndiye aliyewahi
kumnyanyanya mwenzao pikipiki hivyo wakaanza kumshambulia na
kumburuza ambapo hadi jeshi la polisi kufika eneo la tukio mtu huyo
alikuwa tayari ameshachoka na hali yake ilikuwa mbaya wakiwa njiani
kumpeleka hospitali alifariki.
Kamanda
Charles Mkumbo amewataka wananchi kutochukua sheria mkononi kwani
wanaweza kumdhuru mtu ambaye hausiki na tukio amesema kuwa
wanapomuhisi mtu kuwa ni muhalifu watoe taarifa kwa jeshi la polisi
ili sheria ichukue mkondo wake.
Hadi sasa
jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano ambao ni
waendesha pikipiki kwa kuhusika katika tukio hilo,mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya maountmeru ukisubiria ndugu na jamaa
kwenda kumtambua.
0 Comments