Random Posts

NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI, SULEIMAN JAFO AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA CHALINZE NA KUKAGUA SHULE YA SEKONDARI YA MBOGA.

  Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo (mwenye tai) akiingia kwenye kikao kwaajili ya kuzungumza na wadau wa maendeleo na watumishi wa halmashauri ya chalinze, kulia kwake ni Mbunge  wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
 Mbunge  wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akielezea machache kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi  Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo kuzungumza na wadau wa maendeleo na watumishi wa halmashauri ya chalinze.
 Mbunge  wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akimshukuru  Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo kwakuja jimboni kwake.
 Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo alipata nafasi pia ya kutembelea Shule ya Sekondari ya Mboga  ambayo iko katika Ujenzi pia alitazama ujenzi wa Maabara tatu za sayansi zinazojengwa , ujenzi wa madarasa mawili, jiko la kisasa na bwalo na hostel ambazo zitachukua wanafunzi 796.
 Mbunge  wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo kwa  Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo kuhusiana na ujenzi wa hostel unavyoendelea.
 Dada mkuu wa shule ya Mboga sekondari (kulia) akimshukuru  Mbunge  wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete kwa msaada wa kuwatafutia  Hostel na kukamilisha Maabara na kumuahidi watasoma kwa bidii ili asife moyo kuendelea kusaidia katika elimu.
 Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo akiwa na weji wake (kushoto kwake) Mkuu wa Wilaya, Alhaj Majid Mwanga, Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg Zikatimu , na Mbunge  wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukagua shule ya sekondari ya Mboga.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo, Diwani wa Kata ya Msoga na Mbunge  wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakifurahia jambo.

Post a Comment

0 Comments