
Afisa
mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha
ushirikiano baina ya kampuni hiyo na shirika lisilo na kiserikali la
Heifer utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao
wa www.NINAYO.com .Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Heifer International Tanzania Bi. Leticia Mpuya.

Meneja
uendeshaji wa kampuni ya NINAYO Bovan Mwakyambiki akiungumza katika
mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya
kampuni hiyo na shirika lisolo na kiserikali la Heifer International
Tanzania utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao
www.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.

Mkurugenzi
mkazi wa Heifer nchini Bi. Leticia Mpuya akiungumza katika mkutano na
waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya shirika hilo
na kampuni ya NINAYO utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia
njia ya mtandao wa www.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.

Tarehe
22 Machi 2017, Dar es salaam. Kampuni ya Ninayo kwa kushirikiana na
shirika lisilo la kiserikali la Heifer International Tanzania ambalo
limejikita katika kuondoa umasikini na matatizo ya njaa leo
wameshirikiana katika kuwasaidia wakulima wa Tanzania kupata taarifa
zote zinazohusu mauzo au manunuzi ya mazao mbalimbali kupitia mtandao wa
Ninayo.com.
Ninayo
ni jukwaa la mtandao wa kibiashara unaowawezesha wakulima kuuza,
kununua au kuangalia bei elekezi za mazao mbalimbali yatokanayo na
kilimo pia kuwapa uwanja mpana wa kulifikia soko la bidhaa hizo kwa
urahisi.
Njia
hii ya mtandao imejikita katika kutatua mambo makubwa matatu ikiwemo
tatizo la kushindwa kwa mkulima katika usambazaji ambapo
wanunuaji/wateja hawafahamu ni mazao ya aina gani wakulima wanauza,
Mahitaji yasiyofahamika ambapo wakulima hawafahamu ni kiasi gani
wanunuaji wapo tayari kununua mazao yao na kukosekana kwa utaratibu wa
kuwaunganisha wanapohitaji kufanya biashara za mazao yao.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam,
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ninayo Jack Langworthy
alisema matumizi ya intaneti yanazidi kukua kwa kasi sana nchini
Tananzia, na hivi sasa intaneti imesambaa hadi vijiji maskini.
“Tunashukuru
kwa kukua kwa kasi ya mitandao hasa kupitia simu za mkononi, ni
uvumbuzi ambao umeleta mapinduzi katika kila sekta duniani, kuanzia
kwenye bishara ya teksi, hoteli na zaidi sasa inaweza kupatikana kwa
wakulima katika masoko ya Tanzania kukabiliana na mahitaji mahitaji
mbalimbali ya chakula kwa bei elekezi kwa watu wote na hivyo kupunguza
upotevu wa mazao mbalimbali”.
Ninayo
itasaidia kuwaunganisha wakulima kwa pamoja katika soko rasmi, na
itaweka bei elekezi kwenye biashara ya mahindi, maharage, ndizi, maembe,
matikiti maji pamoja na bidhaa nyingine nyingi za kilimo katika kuleta
uwazi na ukweli wa bei ya soko na hivyo kuwawezesha wakulima kujivunia
mazao yao.
Aliongeza
kuwa Ninayo mpaka sasa imefanikiwa kuwaunganisha wakulima wa mikoa kama
Iringa, Mbeya, Morogoro na Njombe pamoja na wanunuaji wa bidhaa zao,
jambo lilisaidia kuongeza kipato chao.
Aliendelea
kusema kuwa Ninayo inaunganisha hadi wakulima wasio na uwezo wa kupata
intaneti kwa kupitia njia ya ujumbe mfupi wa maneno.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Bi. Leticia
Mpuya alipongeza juhudi zinazofanywa kupitia mtandao huo akisema
itasaidia kuwaunganisha wakulima na wateja wao nchini na Afrika
mashariki yote.
Ushirikiano
kati ya Ninayo na Heifer International ni katika kuelimisha wakulima
jinsi ambavyo wanaweza kunufaika kwa kuuza mazao yao kwa kupitia mtandao
huo. Heifer ambao wanafanya kazi na mamia ya wakulima nchini
itawasaidia wakulima wake kutumia mtandao wa Ninayo ili waweze kujipatia
faida kwa kuhakikisha wanauza bidhaa zao kwa bei za kujiridhisha.
“Kama
shirika linalohusika na kutokomeza njaa na umaskini, huwa tunakabiliwa
na changamoto mbalimbali katika kuhakikisha wakulima wanauza mazao yao
kulingana na bei zilizo za kibiashara na kwa manufaa kwao pia kupata
wanunuzi sahihi na hivyo kupitia mtandao huu utasaidia kusulisha
changamoto hiii” alisema.
0 Comments