Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye (aliyekaa kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni wa
China Mhe. DONG WEI (aliyekaa kulia) wakisaini Mkataba wa programu ya
utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu
kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katikati
aliyesimama ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabariel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye (Kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. DONG
WEI (kulia) wakikabidhiana Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala ya
Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi
2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto) akimkabidhi zawadi
ya Kinyago Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Jamuhuri ya watu wa China Mhe. DONG
WEI (kulia) mara baada ya kusaini Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala
ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi
2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye (Kushoto) akizungumza
na Ujumbe kutoka Jamuhuri ya watu wa China pamoja na baadhi ya Watumishi wa
Wizara yake (hawapo katika picha) wakati wa hafla ya kusaini
Mkataba wa programu ya Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya
Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu
Waziri wa Utamaduni Jamhuri ya watu wa China Mhe. DONG WEI.
Naibu Waziri wa Utamaduni Jamhuri ya watu wa China
Mhe. DONG WEI akitoa maelezo mafupi kwa Ujumbe
wa Serikali ya China pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Habari (hawapo
katika picha) katika hafla ya
kusaini Mkataba wa programu ya Utekelezaji
wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia
mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante
Ole Gabariel.
Na Shamimu
Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa
Utamaduni kutoka Jamhuri ya watu wa China
Mhe. DONG WEI wamesaini programu ya utekelezaji wa Mkataba wa masuala ya
Utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 leo Jijini Dar es
Salaam.
Waziri Nape ameeleza kuwa Mkataba huo unalengo
la kuimarisha na kuendeleza ushirikiano
katika Sekta ya Utamaduni ambao umedumu kwa miaka mingi ulioasisiwa na Baba wa
Taifa Mwl.Julius K. Nyerere.
“Tanzania na China
tumekuwa na ushirikiano wa muda mrefu wa masuala mbalimbali ikiwemo hili la
Utamaduni ambalo limetumika kukuza, kulinda na kuunganisha nchi zetu kuwa kitu
kimoja”, Alisema Mhe. Waziri.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI amesema kuwa ushirikiano kati ya
Tanzania na China uliokuwepo kwa muda mrefu
katika masuala ya Utamaduni,
Sanaa, Elimu,Ngoma na Michezo yamesaidia
kuimarisha ushirikiano uliopo na kuwezesha nchi hizi mbili kunufaisha katika
maeneo hayo.
“Ushirikiano wetu wa
muda mrefu katika masuala ya Utamaduni
umeleta mafanikio makubwa ambayo sote tunajivunia kila tunapokuwa
pamoja”.Alisema Mhe. WEI.
Mkataba huo pamoja na
mambo mengine una lengo la kuendeleza na kufanya mpango wa pamoja kwa siku za
usoni, kufanya matokeo makubwa katika Sekta ya Utamaduni kati ya nchi hizo
mbili, Kufanya mkutano maalum wa ushirikiano wakati muafaka, kuzidisha
ushirikiano kwenye sekta ya viwanda katika bidhaa za Utamaduni na Kubadilishana
wataalamu na mafunzo ya kiutamaduni.
Katika hatua nyingine
Serikali hiyo ya China imeisaidia Wizara kiasi cha Yuan laki nne (400,000) kwa
ajili ya kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Wizara.





0 Comments