Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Tanzania
Dkt. Fidelice Mafuniko akisisitiza jambo kabla ya kusainiana hati za
makubaliano kati ya Taasisi hiyo na Shirika lisilo la Kiserikali la Marafiki wa
Watoto wanaoishi na ugonjwa wa Saratani ili kuimarisha uhusiano utakaosaidia
kuwapa fursa ya elimu watoto waliopo Hosipitalini wakisumbuliwa na ugonjwa huo
ili kuwapa haki sawa na wale walio katika mfumo rasmi.kulia ni Mkurugenzi wa
shirika hilo Bw. Walter Miya.
Mkurugenzi wa shirika Shirika lisilo la Kiserikali la
Marafiki wa Watoto wanaoishi na ugonjwa wa Saratani Bw. Walter Miya (kulia)
akizungumza kuhusu umuhimu na Faida za Shirika hilo kushirikiana na Taasisi
hiyo katika kuwawezesha kielimu watoto wanaougua ugonjwa wa Saratani.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima
Tanzania Dkt. Fidelice Mafuniko (kulia) na Meneja wa mradi wa Elimu toka Asasi ya Kimataifa ya
BRAC Maendeleo Tanzania Bw.Abdullah Mahtab wakisaini hati za makubaliano ya
ushirikiano utakaowezesha wasichana
waliokosa fursa hiyo katika mfumo rasmi kupata elimu kupitia mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Tanzania
Dkt. Fidelice Mafuniko (kulia) na Meneja
wa mradi wa Elimu toka Asasi ya Kimataifa ya BRAC Tanzania Bw.Abdullah Mahtab wakibadilishana
hati za makubaliano ya ushirikiano mara baada ya kusaini makubaliano ya
ushirikiano.
Mkurugenzi wa Asasi ya Marafiki wa watoto wanaoishi na
saratani Bw. Walter Miya (kulia) akibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano
na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya watu wazima Dkt. Fidelice Mafuniko.
(Picha na Frank Mvungi Maelezo)
................
Frank Mvungi-Maelezo
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imejidhatiti kuwawezesha
wasichana waliokosa Elimu ya Sekondari katika mfumo rasmi kutokana na kupata
Mimba na Umasikini ili waweze kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa kuwajengea
mazingira ya kupata elimu nje ya mfumo rasmi.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Fidelice Mafuniko wakati wa hafla ya kutiliana saini
makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hiyo na Asasi ya Kimataifa ya BRAC
Maendeleo Tanzania pamoja na Marafiki wa Watoto wanaougua Saratani.
Akizungumzia Makubaliano hayo Dkt. Mafuniko amesema utekelezaji
wa awamu ya kwanza ya majaribio ya mradi wa kuwawezesha wasichana yalikuwa ya
miaka 2 kuanzia June 2014 hadi Machi 2016 ambapo mradi ulitekelezwa katika
Mikoa ya Dar es Salaam, Singida,Shinyanga,Mwanza,Tabora na Tanga.
Katika mradi huo jumla ya wasichana 1,950 wamenufaika na
mpango huo kwa kupata elimu ya Sekondari
kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa katika hatua ya kwanza nakuongeza
kuwa awamu ya pili itahusisha walengwa 300 kutoka Mkoa wa Tanga ambao tayari
wameshasajiliwa.
Awamu ya Tatu inaanza kuteklezwa kuanzia sasa kwa kipindi cha
Miaka 3 na itahusisha wasichana takribani 2000 kutoka katika Mikoa ya Dar es
Salaam,Singida,Shinyanga,Mwanza,Tabora na Tanga.
Mradi huu unatarajia kupanuka zaidi na kuwafikia walengwa
wengi zaidi katika mikoa ya Pembezoni ikiwemo Kigoma,Rukwa na Ruvuma.
Kwa upande wake Meneja wa Elimu kwa Umma kutoka Asasi ya
Maendeleo ya BRAC Tanzania Bw. Abdullaah Mahtab Khan amepongeza mpango huo na
ushirikiano mzuri uliopo kati ya Taasisi hiyo na Asasi yake na kutaka
uendelezwe kwa manufaa ya Watanzania.
Naye Mkurugenzi wa
Asasi ya Marafiki wa Watoto wanaougua Saratani Bw. Walter Miya amesema kuwa asasi
yao inatekeleza mradi wa kuwawezesha watoto wanaougua Saratani kielimu ambapo
hospitali 16 zinatumika.
Alitoa mfano kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
wanafanya kazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
“Asasi yetu imejipanga kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima kuwawezesha watoto wenye saratani kupata Elimu kwani huu ni wajibu
wetu sote kama Watanzania” Alisisitiza Miya.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ilianzishwa mwaka
1960,Pamoja na majukumu mengine ina jukumu la kuratibu na kutoa Elimu ya
Sekondari kwa Vijana na Watu Wazima walio nje ya Shule wenye uhitaji na
waliokosa elimu hiyo.
No comments:
Post a Comment