Wakulima
wanahitaji kuwezeshwa kuendesha kilimo cha kisasa kama hiki ili waweze
kupata mazao ya kutosha na kuboresha maisha yao ,mpango wa TBL Group
kushirikiana na wakulima utasaidia kuleta mabadiliko
Wakulima wanaoshirikiana na TBL mkoani Arusha wakipata maelezo ya kitaalamu katika mashamba yao ya Shahiri.
Kampuni ya
TBL Group imeeleza kuwa pamoja na kuweka kipaumbele utekelezaji mkakati wa
serikali wa ukuzaji sekta ya viwanda nchini
pia itaendelea kushirikiana na wakulima wanaozalisha malighafi kwa ajili ya
viwanda vyake ili kuhakikisha sekta ya kilimo inakua na kutoa mchango
katika pato la taifa ikiwemo kuboresha
maisha ya wakulima nchini.
Hadi kufikia
sasa utekelezaji wa mpango wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wakulima wadogo
wadogo ambao umeanza kutekelezwa na
kampuni hiyo kwa wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania na
wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma umesaidia kuongeza ajira ikiwemo kuboresha
maisha ya wakulima.
Mkurugenzi Mkuu
wa TBL Group ambaye pia ni Mkuu wa
Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin, amesema katika mahojiano
maalumu, kuwa mpango wa kilimo
shirikishi unaotekelezwa katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro mbali na kuinua
hali za maisha ya wakulima pia unanufaisha wananchi zaidi ya 3,000 wanaojipatia
ajira katika utekelezaji wake na kwa upande wa zao la Zabibu zaidi ya
wakulima 700 mkoani Dodoma wamenufaika.
“Moja ya sera ya kampuni yetu ya “Dunia
Maridhawa”-(Better World) inalenga kuwezesha wakulima katika maeneo
tunayofanyia biashara zetu na kuwezesha jamii kuwa na maendeleo endelevu katika shughuli za maisha
yao ya kila siku”.Alisema.
Aliyataja
makundi ya wawaonufaika na mpango huu kuwa ni vibarua wanaofanya kazi
mashambani kwa kupuliza dawa mashambani,madereva wa matrekta wanaolima mashamba
na kuvuna,vibarua wa kupakia mazao na kuyashusha,wasafirishaji na watengenezaji
na magunia ya kupakia mazao.
Alisema Mbali
na wanaonufaika katika hatua mbalimbali
za utekelezaji wakulima wa zao la Shahiri katika mikoa ya Kaskazini ya Arusha
na Kilimanjaro tayari wameanza kuonja
matunda ya ushirikiano huu kwa kuwa wanawezeshwa kuendesha kilimo cha
kisasa,kupatiwa pembejeo,mbegu na wataalamu wa kutoa ushauri na wanakuwa na
soko la uhakika kwa ajili ya kuuza mazao yao,hali ambayo imebadilisha hali zao
za maisha kuwa bora.
“Mpango wa
kampuni wa kushirikiana na wakulima haulengi kunufaisha wakulima wa Shahiri na
Zabibu pekee bali pia wa mazao mengine kama mtama na mihogo na katika siku za
usoni wakulima wa zao la mahindi watawezeshwa pia na wananchi wengi watajipatia riziki kutokana na kufanya
kazi za utekelezaji wake”.Alisema
Mpango huu wa
kampuni kutegemea kupata malighafi kutoka
hapa nchini umeungwa mkono na serikali za nchi mbalimbali ikiwemo
Tanzania kwa kuwa unalenga kuinua hali za maisha za wananchi hasa wakulima
ambao wana hali duni kutokana na changamoto nyingi zilizopo katika sekta ya
kilimo.
Huu ni mfano
wa uwekezaji wenye faida kwa watanzania kwa kuwa unaeleta mabadiliko kwenye
jamii na kubadilisha maisha ya wananchi wengi kuwa bora.





0 Comments