Na Magreth Magosso, Kigoma
Wanafunzi
wanaosoma katika Shule ya Msingi Munyika Kijiji cha Kajana tarafa ya
Muyama wilayani Buhigwe mkoani kigoma wamekubwa na ugonjwa wa ajabu hali
iliyowalazimu wazazi na walezi kufika shukeni hapo kwa ajili ya
kuwapatia tiba mbadala na wengine 80 wapelekwa katika Zahanati ya Kijiji
hicho baada ya kuzidiwa na maumivu ya kichwa, tumbo huku joto la miili
yao ikiongezeka kila mara.
Akithibitisha
hilo kwa njia ya simu, Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mnyika Japheti
Lukanka alikiri kutokea kwa tukio hilo, ambalo limejitokeza machi 6,
mwaka huu, saa 1:30 asubuhi , hali iliyowalazimu baadhi ya wazazi
kuwaombea ruhusa watoto wao wanaosoma katika shule hiyo ili kuwapatia
matibabu.
Lukanka alisema
kuwa wakiwa paredi katika zoezi la ukaguzi wa usafi , ghafla mwanafunzi
mmoja alidondoka na kupewa huduma ya kwanza hatimaye alirudishwa
nyumbani kwao kitendo kilichozidi kuwashtua ni pale wanafunzi wa darasa
la sita walienda ofisini kwakwe na kuomba ruhusa kwa kuugua ugonjwa huo
na kufika saa 6.00 mchana idadi ya wanafunzi waliokutwa na hilo walikuwa
zaidi ya 80.
Akithibitisha
kuwapokea wagonjwa hao Ofisa Tabibu wa Zahanati ya Kijiji cha Kajana
Festo Eliakimu akiri kupokea wanafunzi 70 wakiwa na hali mbaya na
kuwapatia huduma ya kwanza lakini alikabiliwa na tatizo la ukosefu wa
kipima joto (thermometer) , hali iliyomlazimu aombe kipimo hicho kwa
ofisa afya wa Wilaya ya Buhingwe.
“chanzo
cha ugonjwa hakijajulikana mapaka leo na wanafunzi 70 nimewapumzisha na
kuwapatia huduma ya kwanza, hapa sina vipimo vya joto hivyo nimeomba
msaada kwa afisa afya wa Wilaya na amekwisha fika hapa japo baadhi ya
wazazi wamewachukua watoto wao na kuwapeleka Hospitali ya shunga ambayo
ina vipimo zaidi , baada ya kuona hali zao zinazidi kuwa mbaya” alieleza
Eliakimu.
Kwa niaba ya
wazazi wa watoto hao Violethi John alisema tukio hilo limewashangaza kwa
kuwa ni mara ya kwanza kuona watoto wao wanaumwa wakiwa shule, na
kuupongeza uongozi wa shule hiyo, zahanati na Wilaya hiyo kwa
ushirikiano walioutoa katika kuokoa maisha ya wanafunzi hao.

0 Comments