Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, meja Jenerali Gaudence S.Milanzi alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kufunga ya wiki sita ya kuwaanda watumishi ambao ni Maafisa wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania-TAWA kuingia kwenye mfumo wa kijeshi (Jeshi usu) katika hafla iliyofanyika kwenye kituo cha mafunzo kilichopo wilayani Mlelelemkoani Katavi. Mafunzo hayo yalianza Januari 30,mwaka huu kwa maafisa 100 kati yao,99 walikuwa ni kutoka TAWA na mwingine ni ofisa kutoka TANAPA waliyokuwa tayari kwa majukumu waliyopangiwa.
0 Comments