Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
mara baada ya kumaliza mazungumzo na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel
Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki
maarufu kama Ney wa Mitego akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisalimiana na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya
Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa mwaliko Ofisini kwake Mjini Dodoma
kufanya mazungumzo yahusuyo mambo ya Sanaa ya Muziki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki
maarufu kama Ney wa Mitego akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt
Harrison Mwakyembe Mjini Dodoma kwa mazungumzo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa Msanii wa Muziki wa kizazi
kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego mara baada ya mazungumzo
Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
.............
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa wasanii nchini kutovuka mipaka katika utengenezaji
wa kazi zao mpaka kufikia hatua ya kuvunja Sheria na taratibu za nchi.
Ameyasema hayo Mjini Dodoma jana alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Msanii wa muziki wa
kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa mwaliko wa Waziri
huyo.
Amesema kuwa
wasanii ni nguzo muhimu katika nchi sio kwa kufanya kazi ya kuburudisha na kuelimisha bali katika
kuujenga Utamaduni wa nchi ambao ndio nguzo muhimu sana kwa malezi na makuzi ya
wanajamii.
“Niwaombe wasanii nchini kuzingatia Sheria na
taratibu za nchi katika utunzi wao na utenegenezaji wao wa kazi zao”
Alisisitiza Mhe. Dkt Mwakyembe.
Aidha ameongeza kuwa Serikali haina nia ya
kuwanyima uhuru wa kujieleza bali watambue kuwa nchi inaendeshwa kwa taratibu
na Sheria ambazo zinatakiwa zifuatwe na watu wote.
Kwa upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya
Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuwaunga mkono wasanii nchini na kuahidi
kuongeza baadhi ya mambo katika wimbo wake wa “Wapo” na kuwaalika watanzania
kama kuna kero zingine zinazowasumbua katika jamii wasiwasilishe kwake ili azizungumzie
katika wimbo huo.
“Namshukuru Mhe. Rais kwa kutuunga mkono pia
naahidi kufanya “remix” ya wimbo wa “Wapo” kwa kuongeza maneno niliyoshauriwa
na Mhe Rais na Mhe. Waziri na kama kuna mengine kutoka kwa wananchi pia niko
tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi” alisema Bw. Elibariki.
Hivi karibuni wimbo wa “Wapo” wa Msanii Emmanuel
Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego ulifungiwa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) kwa kosa la kutozingatia maadili na baadae kufunguliwa kwa agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kupitia Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe.






0 Comments