Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof.Jumanne
Maghembe (katikati) akizungumza na wananchi kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya
miaka 110 ya vita vya Maji Maji na uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Rashidi
Kawawa yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Wengine ni Mkuu wa
mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge ( wa pili kulia) Mbunge wa viti maalum wa
Ruvuma, Jacquiline ngonyani ( wa kwanza kulia) Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania, Egon Kochanke ( wa kwanza kushoto) pamoja na Chifu wa wangoni,
Emanuel Zulu (wa pili kushoto) .
Picha na Lusungu Helela- WMU)
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof.Jumanne Maghembe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge
wakiangalia baadhi ya Nishani alizokuwa akitunukiwa Dkt. Rashid Mfaume Kawawa
katika kulitumikia taifa kwa uzalendo mara baada ya kuzinduzia jana Makumbusho ya Hayati
Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea.
Picha na Lusungu Helela- WMU)
Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke akiweka taji kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa
waliouawa kwa kunyongwa na wakoloni kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji
Majiyaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea.
Picha na Lusungu Helela- WMU)






0 Comments