Faida ya Hifadhi endelevu ya Mazingira. Pichani
ni eneo la Ngaresero Wilaya ya Meru ambapo kuna uhifadhi mzuri wa mazingira.
Hata hivyo eneo hilo limeanza kuvamiwa na wananchi kwa shughuli za kibinadamu
na kuhatarisha uhai wake. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo na kumtaka Bw.
Timoth Leach mmiliki wa Ngaresero Mountain Lodge kufanya ukaguzi wa mazingira
mara moja ili kubaina matumizi sahihi ya rasilimali maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati
Edward Moringe Sokoine. Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi Mkoani
Arusha na alitembelea msitu wa Enguiki na Lendikinya kisha alizungumza na wananchi
katika mkutano wa hadhara.


0 Comments