
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye
ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na katikati ni
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye
ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri.


Baadhi
ya wadau wa zao la tumbaku wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim majaliwa
wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Machi, 16, 2017.

Mwenyekiti
wa WETCU, Gabriel Mukandara (katikati) na Makamu wake, Msafiri Ngassa
wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamis Issah (kulia)
kuelekea kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji
wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la
tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16,
2017.

Mwenyekiti
wa WETCU, Gabriel Mukandara na Makamu wake, Msafiri Ngassa (kushoto)
wakiwa kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji
wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la
tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16,
2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora
kuwakamata viongozi wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU)
pamoja na kufunga ofisi za chama hicho hadi uchunguzi wa tuhuma za
ubadhirifu wa fedha za chama hicho utakapokamilika.
Pia
Waziri Mkuu amevunja Bodi ya WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania
- TTB kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi
mabaya ya fedha za umma.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo leo jioni (Alhamisi Machi 16, 2017) katika
kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora,
ambapo amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa
Mwenyekiti wa TTB, Bw. Vita Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo
Bw. Wilfred Mushi.
Viongozi
wa WETCU ambao Waziri Mkuu ameagiza wakamatwe ni Mwenyekiti Bw.
Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa
Ndani na Mhasibu Mkuu. Pia amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha
uhasibu wa chama hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.
“Kuanzia
sasa watumishi wote wa kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti
nimewasimamisha kazi pamoja na Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius
Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo
timu ya ukaguzi itakapokamilisha kazi yake,” amesisitiza.
Waziri
Mkuu amesema kwa muda mrefu wakulima wameteseka na zao hilo kukosa tija
kwa sababu ya usimamizi mbovu wa viongozi wa ushirika na Bodi ya
Tumbaku Tanzania jambo ambalo Serikali haiwezi kulivumilia.
Amesema
“Hatuwezi kuwa na ushirika ambao hauwasaidii wanachama. WETCU walipokea
sh. bilioni 15 ambazo walizikatia risiti na hazijaonekana. Pia
waliwalipa wazabuni sh, bilioni 10 ambazo hawajazikatia risiti,”.
“Wakati
wanachama ambao ni wakulima wakiendelea kutesema WETCU walinunua gari
la sh. milioni 269 kinyume na na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa wadau
ambao ulipitisha zitumike Shilingi milioni 40 tu,” amesema.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa chama hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji
kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo
limechangia wakulima wa tumbaku kukosa tija.
Amesema
WETCU kimekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha ambapo alitolea mfano
suala la ukarabati wa ofisi tatu ikiwemo ya makao makuu ambayo ilipangwa
ikarabatiwe kwa sh. milioni 33 wakatumia sh. milioni 170 na ofisi za
Tabora na Urambo zilipangiwa sh. milioni tano kila moja na
hazikukarabatiwa.
Pia
Waziri Mkuu amepiga marufuku ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi
wkatiikiwa inazalishwa hap nchini. Aidha, alimepiga marufuku matumizi ya
kwa dola katika sekta ya tumbaku na badala yake zitumike fedha ya
Kitanzania kwa sababu kitendo hicho kimekuwa kiwanyonya wakulima.
Katika hatua nyingine
Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Aggrey
Mwanri, wakuu wa wilaya zote za mkoa huo pamoja na Maofisa Kilimo na
Ushirika kuhakikisha wanasimamia vizuri zao hili ili liweze kuwa na tija
kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Pia
amewaagiza Maofisa Kilimo waende vijijini na kuwatambua wakulima wa
tumbaku katika kila kijiji na kuwasajili. “ Kuanzia leo Maofisa Ushirika
wabadilishe mienendo ya kazi nataka wasimamie zao la tumbaku kwa
umakini zaidi.”
0 Comments