Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akitazama baadhi ya vifaa
vya kisasa vilivyofungwa katika hospitali hiyo,alipotembelea mapema leo
kuangalia vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Koica Chanika, jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya Vifaa vya kisasa ambavyo tayari vimeishafungwa katika hospitali hiyo.
Majengo ya hospitali hiyo kama yaonekanavyo pichani, iliyojengwa
kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini,ampapo inatarajiwa kuzinduliwa
Juni 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsikiliza Mganga wa
Manispaa ya Ilala,Willy Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo
ya vifaa mbalimbali vilivyofungwa katika hospitali hiyo mapema leo
jijini Dar,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema.
.....
Katika kutimizwa kile kinachoitwa
Deni la serikali ya Mkoa kwa wakazi wake wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa
Mh Paul Makonda leo hii ametembelea ujenzi wa Hospitali ya KinamMkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akitazama baadhi ya vifaa vya
kisasa vilivyofungwa katika hospitali hiyo,alipotembelea mapema leo
kuangalia vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Koica Chanika, jijini Dar
es Salaam.
Ujenzi huo ambao ulizinduliwa kwa
kuwekewa jiwe la msingi na Mh Paul Makonda mwanzoni mwa mwaka jana
baada ya ombi la ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya mama na mtoto kwa
wakazi wa Dar es salaam kupokelewa na kukubaliwa na ubalozi wa Korea
kusini hapa nchini.
Ukamilishwaji wa ujenzi huu
unasindikizwa pia na ujenzi wa nyumba 28 za makazi kwa ajili ya wauguzi
na madaktari watakaohudumu hospitali hiyo masaa 24.
Ukamilishwaji wa ujenzi huu ambao
hadi sasa umebakiza hatua ya mwisho ya ufungaji wa vitanda 160 vya
wagonjwa na 10 vya kujifungulia wakina mama wajawazito pamoja na vifaa
inaendelea kwa sasa. Ni uthibitisho tosha wa kuonesha nia ya dhati ya
Serikali ya Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha huduma bora za kiafya
zinawafikia wananchi wote wa Tanzania kwa wakati.
Hospitali hii ya kihistoria na
aina yake itakuwa ni mahusisi kwa wakina mama na Watoto wa Mkoa wa Dar
es salaam na wamama wote wa maeneo jirani na inatarajiwa kufunguliwa
mwezi Juni mwaka huu (2017) na Mh rais wa JMT DrJohn Pombe Magufuli.
Pongezi nyingi zimfikie Mh Paul
Makonda na Wataalam wake kwa jitihada za kutatua changamoto mbalimbali
za wananchi wa Dar es salaam kwa kishirikiana na wadau mbalimbali wa
maendeleo hapa nchini.





0 Comments