Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro akikagua gwaride la heshima la kikosi cha jeshi la anga la Ireland
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro akimkabidhi Rais Michael D. Higgins hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe.Rais John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro akiagana na Rais Higgins.
Michael D. Higgins akimuaga Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro baada ya kupokea hati yake ya utambulisho
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro alikutana kwa mazungumzo na wanadiaspora wa Tanzania waishio katika miji mbalimbali ya Ireland.
...........
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose
Migiro mapema mwezi huu aliwasilisha hati ya utambulisho (letter of
credence) kwa Rais wa Ireland, Mhe. Michael D. Higgins.
Akiwasilisha
hati hiyo katika Ikulu ya Ireland, Balozi Migiro alimfikishia Rais
Higgins salam za Mhe. Rais John Magufuli na wananchi wa Tanzania pamoja
na kumuahidi kufanya kazi itakayoimraisha uhusiano wa kihistoria baina
ya Serikali za Tanzania na Ireland pamoja na kuanzisha maeneo mapya ya
ushirikiano kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano ya
kujenga uchumi wa viwanda. Kabla ya kuagana na Rais Higgins, Balozi
Migiro alikagua gwaride rasmi liliondaliwa na kikosi cha Jeshi la Anga
la nchi hiyo.
Akiwa Ireland, Balozi Migiro pia alikutana kwa mazungumzo na wanadiaspora wa Tanzania waishio katika miji mbalimbali ya Ireland.
Katika
mkutano huo aliwasihi wanadiaspora kushikamana, kuwa wamoja na kuunda
Jumuiya ya Watanzania waishio Ireland akiwakumbusha kauli ya wahenga
isimayo kuwa 'Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu'.






0 Comments