Jumanne Aprili 25, 2017 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt
Asha-Rose Migiro, amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki
Ibada Maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la
Westminster Abbey jijini London.
Ibada
hiyo ilifanyika kama sehemu ya kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar. Ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola, Tanzania
hufanyiwa maombi maalum kanisani hapo katika siku hii adhimu kila mwaka.
Pamoja
na kusoma maandiko matakatifu, Ibada hiyo ilihusisha maombi maalum kwa
ajili ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake, Mahakama na
Bunge kama mihimili mikuu ya Amani na Mshikamano wa Taifa la Tanzania na
Wananchi wote wa Tanzania ndani na nje ya Nchi.
Ubalozi
wa Tanzania London Uingereza unawatakia kheri Watanzania wote waishio
Uingereza na Jamhuri ya Ireland katika maadhimisho ya miaka 53 ya
Muungano wa Taifa letu.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt Asha-Rose Migiro, akiwa
amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki Ibada Maalum ya
kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la Westminster Abbey
jijini London leo.


0 Comments