Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Majid Mwanga, mwenye T-shirt lenye rangi nyekundu, akitembelea miundombinu mbalimbali hususan ya barabara iliyoharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
..
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo,mkoani Pwani alhaj Majid Mwanga,amesema
nyumba zaidi ya nyumba 100
zilizopo kata ya Bwilingu,eneo la Chalinze Mzee na kata ya Msoga zimeharibika
,kubomoka na nyingine kuezuliwa mapaa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kufuatia maafa hayo ,amewaomba wadau mbalimbali wa jamii
kujitokeza kusaidiana na serikali kuwasaidia wahanga wa mafuriko yaliyotokana
na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia april 7 hadi 8.
Aidha alhaj Mwanga, ametoa rai kwa jamii kuendelea kusaidiana kwa
sasa wakati serikali ikiendelea kutafakari namna ya kushirikiana na wadau .
Mvua hizo zimeathiri baadhi ya maeneo ya Msoga,Chalinze
Mzee,darasa moja katika shule ya msingi Kidogozero, Bwawa la umwangiliaji la
Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.
Akizungumza na baadhi ya wakazi waliokumbwa na maafa hayo na
waandishi wa habari, mara baada ya kutembelea maeneo hayo,alhaj Mwanga ,
alisema kwasasa majirani,ndugu na jamaa waendelea kusaidiaana .
Alieleza kuwa hatua zitakazofuata zitakuwa ni ziada pekee lakini
haina budi kusema ukweli kuwa kilichopo sasa ni jamii kusaidia yenyewe kwa
yenyewe.
“Serikali inatafakari cha kufanya kutafuta wadao,ila tuende na
ukweli lazima muhakikishe mnasaidiana wenyewe kwa wenyewe pasipo kuitegemea
serikali pekee”
“Nashukuru hakuna maafa makubwa makubwa ya vifo na majeruhi zaidi
ya kubomoka kwa nyumba na
kuharibika ambapo wahusika wamepata hasara kubwa”alieleza alhaj Mwanga.
Baadhi ya wakazi akiwemo mzee Rashid Mwinyigoha ,alisema mvua hiyo ni kubwa na
haijawahi kutokea ambayo imewapa hasara kubwa.
Alibainisha kuwa hali hairidhishi kwani nguo,fedha,chakula na vitu vyote vimeondoka na maji
hivyo hawana la kufanya.
Kwa upande wa watoto wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Chalinze
mzee wanaiomba serikali na wafadhili kuwawezesha vifaa vya shule ikiwemo
madaftari,sare za shule na viatu ambavyo vimesombwa na vingine kuharibiika kwa
mvua.
Diwani wa kata ya Bwilingu ,Lucas Rufunga ,alisema amepokea janga
hilo kwa masikitiko makubwa na sasa wameshaanza kufanya tathmini ya awali kwa
kupita nyumba hadi nyumba lakini hawajafanya tathmini ya hasara iliyopatikana .
Alisema nyumba zilizoharibika kiasi,zilizobomoka zaidi ya 100
ambapo ndani hakujabaki kitu kwa kupata hasara ya kuharibiukiwa na vitu vyao.
“Huwezi kujua nyumba hii au hiyo imegharimu kiasi gani kama risiti
zinazoonyesha vifaa vya nyumba walivyonunua havipo hivyo tumefanya tathmini ya
nyumba zilizobomoka na kuharibika”alisema Rufunga.
Kwa upande wake ,katibu wa mbunge wa jimbo la Chalinze,Idd Swala,alisema
Ridhiwani Kikwete anatarajia kushirikiana na diwani wa kata hiyo kusaidia
wanafunzi ambao vitu vyao vya shule vimeharibika na mvua na vingine kusombwa na
maji.
Ridhiwani atakachokifanya ni kuangalia namna ya kuwezesha sare kwa
baadhi ya wanafunzi hao na madaftari ili kuhakikisha watoto wanaendelea na
masomo baada ya sikukuu ya pasaka.




0 Comments