Bw. Salaam Mendes akitaja bei ya pafyum hiyo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi leo jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha chupa ya pafyum ya CHIBU aliyoizindua leo jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akimkabidhi chupa
ya Pafyum Aisha Azori mteja wake wa kwanza aliyenunua bidhaa hiyo kwenye
maduka ya GSM Mall jijini Dae salaam.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha Pafyum ya CHIBU ambayo ndiyo kwanza imeingia sokoni.
Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akizungumza na
waandishi wa habari wakati akizindua Pafyum hiyo kulia ni Mmoja wa
Mameneja wake Babu Tale.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka
Diamond Plutnamz akiwasili kwenye maduka makubwa ya GSM Mall Barabara ya
Nyerere leo tayari kwa kuzindua Pafyum yake inayoitwa (CHIBU), Diamond
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo amesema
ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza pafyum zenye nembo yake CHIBU
ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba
wa ajira nchini.
Ameongeza kwamba kuanza
kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi
lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa
kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza
kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na
itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika mkakati mwingine wa soko
Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo
na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili
ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa
ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege
katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika








0 Comments