Mkurugenzi wa Ikolo Investment Ltd Magidd
Mjengwa akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili kuhusu nafasi yao
katika kukuza uchumi wa Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora
Tanzania Mwinyimkuu Khatibu.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora Tanzania
Mwinyimkuu Khatibu akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili kuhusu
nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania.Kushoto ni Mkurugenzi wa Ikolo
Investment Ltd Magidd Mjengwa
Msanii marufu wa Kundi la Orijino Komedi
Emmanuel Mgaya (maarufu Masanja Mkandamizaji) akielezea jambo wakati wa
Kongamano la Diaspora akizungumza wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili
kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Ikolo Investment Ltd Magidd Mjengwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Diaspora
Tanzania, Mwinyimkuu Khatibu (kushoto). Kongamano hilo la siku mbili pia
linatumika kuadhimisha miaka 10 ya Mjengwa Blog iliyoanzishwa mnamo tarehe 19,
Septemba, 2006.
Mtanzania anayeishi nchini Denmark Bi. Edith
Chenga akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Diaspora kujadili kuhusu nafasi
yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo
la siku mbili linafanyika katika Ukumbu wa Makumbusho ya Taifa linatarajiwa
kumalizika kesho tarehe 12 Aprili 2017.
Msanii marufu wa Kundi la Orijino Komedi
Emmanuel Mgaya (maarufu Masanja Mkandamizaji) akiwa na baadhi ya washiriki wa
Kongamano la Diaspora lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kujadili nafasi ya Diaspora katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Mjasiriamali
wa bidhaa za Dagaa Fresh wa kutoka Ziwa Victoria ambaye pia Mkurugenzi wa
Kampuni ya Winlab Bi. Winfrida Simo Tlatlaa akielezea baadhi ya washiriki wa
Kongamano la Diaspora kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo
Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akijisajili kwa ajili ya kushiriki Kongamano
la Diaspora kuhusu nafasi yao katika kukuza uchumi wa Tanzania leo Jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wawasilisha mada wakiendelea na majadiliano wakati wa Kongamano la Diaspora kuhusu nafasi ya Diaspora katika kukuza uchumi wa Tanzania katika Kongamano lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.










0 Comments