WATANZANIA wametakiwa kuingia katika ubia kama wajasiriamali
badala ya kufikiria kwamba wao ni maskini na hawana fedha za kuingia
ubia na makampuni ya nje.
kauli hiyo imetolewa katika wiki ya Ufaransa ambapo makampuni
50 yanashiriki kuonesha uwezo wa utayari wa ushiriki wao katika ujenzi
wa uchumi wa kati wa Tanzania unaotegemea viwanda.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk.
Reginald Mengi ambaye aliwasilisha haja na matamanio ya Watanzania
kwenye sekta binafsi katika kushirikiana na wawekezaji kutoka Ufaransa,
alisema watanzania wamekuwa waoga kuomba ubia wakidhani kwamba hawana
kitu cha kutoa wakati wao wana akili na rasilimali.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi
akizungumza katika kilele cha wiki ya Ufaransa ambapo wawekezaji kutoka
makampuni 50 ya Ufaransa walishiriki katika mkutano huo uliofanyika
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliombatana na maonesho ya bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa na wafaransa.
(Picha zote Thebeauty.co.tz)
Kauli hiyo ambayo aliisema kwenye mazungumzo na wawekezaji
hao wa Ufaransa wakati akielezea utayari wa sekta binafsi kushirikiana
na Wafaransa alisema kwamba watanzania wengi hawajiamini na kwamba
wakati umefika kwa Watanzania kujitambua kwa kuwa wao (wafaransa)
walijaribu wakaweza kwani kama sisi walikuwa na vitu vya ziada katika
uthubutu wao.
Katika mazungumzo yake Dk. Mengi akiwa pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema kwamba sekta binafsi ambayo
ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi inawezekana kwa watanzania
kuthubutu.
Aidha alisema uwapo wa Wafaransa utaweza kusaidia kupandisha
uwezo, teknolojia na utaalamu hali ambayo inawezekana kupitia uwapo wa
shughuli za ubia kati ya wawekezaji wa Kitanzania na Wafaransa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye
(kulia) akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika
mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano
wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana
jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Alisema baada ya sekta ya umma kuweka miundombinu mahala
pake, ni kazi ya sekta binafsi kutumia miundombinu hiyo kubuni na
kuwekeza katika viwanda na kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Dk.Mengi alisema kwamba TPSF inaamini kwamba sekta binafsi ni
ufunguo katika kuongoza na kuimarisha uchumi wa Tanzania ambao
unatakiwa kuwa endelevu kama awamu ya tano inavyotaka.
Aliwaambia wafanyabiashara wa Ufaransa kwamba Tanzania ina
kila kitu wanachohitaji na kwamba makampuni makubwa ya Ufaransa kama
Airbus, Renault, Alstrom, Systra wana mtandao mpana duniani wa
kufanyabiashara na wawawekezaji wadogo duniani hivyo wanaweza kufanya
hivyo hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akiuliza swali kwa Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (hayupo
pichani) wakati wa mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga
kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa.
Alisema changamoto za utaalamu zitaondoka kwa ushirikiano na uwezeshaji.
Aliwataka wawekezaji hao wa Kifaransa kwamba Tanzania kwa
sasa ndio nchi ya uwekezaji na kusema changamoto zilizopo ni fursa za
uwekezaji nchini Tanzania hasa katika nishati ambapo taifa hili
litahitaji megawati 10,000 ifikapo mwaka 2040.
Aidha alisema anaamini kwamba wengi wa watanzania wapo tayari
kushirikiana na Ufaransa katika kuhakikisha kwamba wanaingia ubia
katika biashara halali na yenye kusaidia pande zote.
Naye Simbeye alisema anatamani kuona kwamba wafaransa
wanawekeza kiwanda cha magari nchini kwani inawezekana kutokana na
mabadiliko makubwa ya mfumo wa uwekezaji kwa sasa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk.
Reginald Mengi akifafanua jambo katika mkutano huo kwenye kilele cha
wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji
kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Mmoja kati ya wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa akiuliza
swali kwa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) katika kilele cha
mkutano wa wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es
Salaam.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
(TSPF) Dk. Reginald Mengi, Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak
pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira katika
mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika ukumbi wa
makumbusho ya Taifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili
kulia) pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara walioshiriki mkutano huo
wa kilele cha wiki ya Ufaransa iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho
ya Taifa.
Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara katika
Ubalozi wa Ufaransa nchini, Blevin Claude (wa pili kushoto) akiwa na
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Uchumi katika Ubalozi wa Ufaransa
nchini, Beatrice ALPERTE (kushoto) katika mkutano huo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali
wanaochukua masomo ya biashara walioshiriki mkutano wa kilele cha wiki
ya Ufaransa uliofanyika katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau na wafanyabiashara kutoka makampuni 50 ya nchini Ufaransa walioshiriki mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Sales Executive wa kampuni ya CMC Formula wauzaji wa magari ya
Renault, Erica George akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati akitembelea mabanda
katika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa iliyofanyika kwa mara ya kwanza
nchini katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akipata maelezo katika banda la kampuni ya TOTAL.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya AIRBUS HELICOPTERS, Jean-Marc Royer
(kulia), akitoa maelezo ya shughulli wanazofanya kwa Mwenyekiti wa
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (wa pili
kushoto) alipotembelea mabanda ya kampuni mbalimbali kutoka nchini
Ufarasan zilizoshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Ufaransa
yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam
Kushoto ni Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi
wa Ufaransa, Blevin Claude.
Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya
biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude akitoa neno la shukrani kwa
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati
Dk. Mengi akijiandaa kuondoka katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
yalipofanyika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa jijini Dar es Salaam.
















0 Comments