Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, wa kulia akishiriki kushusha mifuko ya saruji ambayo itatumika katika ujenzi wa soko la Mlandizi ambapo ndio ameanza maandalizi ya ujenzi utakaogharimu mil. 180,awamu ya kwanza itatumia mil. 50.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, akishiriki kuchimba mashimo ya maandalizi ya ujenzi wa soko Mlandizi.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,wa kwanza kushoto akisaidia kushika kamba kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa soko Mlandizi.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Vijijini
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,
Mkoani Pwani, Hamoud Jumaa, amesema 2017/2018,anajikita kutekeleza ahadi na
vipaombele alivyojiwekea kwenye za huduma za kijamii hasa afya ,elimu na soko.
Katika utekelezaji huo, ameanza
maandalizi ya kujenga soko la Mlandizi awamu ya kwanza litakalogharimu mil. 180
hadi kukamilika kwake.
Jumaa alisema watafanya ujenzi kwa
awamu ambapo awamu ya kwanza itagharimu mil. 50.
Alieleza kuwa, soko la Mlandizi ni
soko linalotegemewa na wakazi wengi wa mji huo hivyo kuna kila sababu
kulijengea mazingira bora na kuwa la kisasa .
Aidha Jumaa alisema ,wafanyabiashara
wamejipanga kumuunga mkono kwa kuchangia sh. 5,000 kila mmoja ambazo zitakuwa
zikichangishwa kupitia ofisi ya soko.
"Simaanishi kuwa hakuna kero
nyingine lakini ninafanya kwa awamu na mengine ninatekeleza pale napopata fedha
ama wafadhili na wadau mbalimbali "alisema Jumaa.
Jumaa alibainisha, masuala hayo ni
utekekelezaji wa ilani ya CCM na atahakikisha hadi ifikapo 2020 awe amemaliza
ahadi zake na vipaombele alivyojiwekea.
Mbunge huyo alisema,ni jukumu lake
kuwatumikia wananchi na aliwaomba washirikiane kwa kufuata kauli mbiu yake ya
SISI KWANZAA SERIKALI BAADAE.
Katika hatua nyingine - afya
anaendelea na ujenzi wa uzio katika Kituo cha afya cha Mlandizi ambao unaenda
vizuri.
Jumaa alifafanua kwenye
mfuko wa jimbo atachangia sh. mil. 4 kununulia tofali, wadau wameshamkabidhi
mifuko 500 ya saruji iliyogharimu sh. mil. 6, kokoto tani 7 kwa sh. mil. 9.1,
mchanga mil. 2.4 tofali sh. mil 8.4, na nondo tani moja sh. mil. 3.6.
Alieleza ujenzi huo
utagharimu mil. 200 utafanyika kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza itatumia
sh. mil. 40.
"Niwaombe wadau
mbalimbali wa maendeleo na serikali kuendelea kuniunga mkono ili Kibaha
Vijijini ipige hatua ya kimaendeleo na kiuchumi "alisema.
Diwani wa kata ya
Mlandizi Ephrasia Kadala ,alisema madiwani watachangia 240,000 kila mmoja.
Nae makamu mwenyekiti wa
halmashauri, Godfrey Mwafulilwa walimpongeza Jumaa kwa kasi na juhudi
zake na kusema halmashauri ipo nae bega kwa bega .
Hivi karibuni mbunge huyo
alitoa viti 18 vya kubebea wagonjwa vilivyogharimu mil 5.4,vifaa tiba na
machine ya kupumulia vya mil. 11 katika Kituo cha afya Mlandizi.
Alitoa pia kontena la
vitabu 4,000 vya kujifunzia lililogharimu mil. 66 vitabu ambavyo vilisambazwa
katika shule za msingi na sekondari halmashauri ya wilaya ya Kibaha .




0 Comments