Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu akitoa
ufafanuzi wa Utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa Bajeti ya mwaka 2016/17
katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, wakati wa
mapitio ya Bajeti ya mwaka 2017/18 kwa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Kamati hiyo chini ya Uenyekiti wa Mhe.
Musa Azzan Zungu (Mb, wa pili kulia) imejadili na kuridhia Taarifa ya bajeti ya
Wizara hiyo siku chache kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
linalotarajiwa kuanza mapema mwezi Aprili, 2017. Kushoto, anayefuatilia maelezo
ni Naibu Waziri Mhe. Hamisi A. Kigwangalla (Mb). Kikao
hicho kilianza tarehe 31 Machi na kuhitimishwa tarehe 1 Aprili, 2017 katika
ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Wa pili kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Musa Azzan
Zungu (Mb) akiongoza majadiliano ya kikao cha Kamati hiyo kilichokutana UDOM Dodoma
kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2017/18 kwa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na taasisi zilizochini ya Wizara
hiyo na kupitia Mpango wa bajeti kwa mwaka 2017/18. Wa pili kushoto ni Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu akifuatilia
mwenendo wa kikao, na kushoto ni Naibu Waziri Mhe. Hamisi A. Kigwangalla (Mb). Kamati imeipongeza Wizara kwa
jitihada zinazofanyika katika kutekeleza majukumu ya kisekta na imeridhia
Bajeti ya Wizara kwa hatua zinazofuata.
Kulia ni Mhe. Hamisi A. Kigwangalla (Mb) akifuatilia kwa makini maelezo
ya Mhe. Waziri (Hayupo pichani) kuhusu Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikiwasilishwa na
Mhe. Waziri (Hayupo pichani). Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara
kuu ya Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba S. Nkinga na
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara Idara kuu ya Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya.
Wakifuatilia Taarifa inayowasilishwa kwa wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii katika kikao cha siku mbili
kilichofanyika Chuo kikuu cha Dodoma na kuhitimishwa leo mchana.
Kulia ni Katibu Mkuu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Idara kuu ya Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bibi Sihaba S. Nkinga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara Idara kuu ya Afya Dkt.
Mpoki Ulisubisya. Wakisikiliza na kunukuu
maelezo ya hoja zilizotolewa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Maendeleo ya Jamii katika kikao cha siku mbili kilichofanyika Chuo kikuu cha
Dodoma na kuhitimishwa leo mchana. Kushoto ni mmoja wa waheshimiwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jmaii.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii wakipitia
Taarifa za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
iliyowasilishwa na kujadiliwa kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa Chuo
Kikuu cha Dodoma na kuhitimishwa leo tarehe 1 Aprili, 2017. Taarifa hiyo
imepitishwa kwa hatua za maandalizi ya
vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajiwa kuanza mapema mwezi Aprili, 2017.
Wengine katika mstari wa nyuma ni Watendaji
waandamizi wa Wizara hiyo. Kikao hicho
kilianza Alhamis tarehe 31 Machi na kuhitimishwa tarehe 1 Aprili, 2017
katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodom
Baadhi ya waheshimiwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya
Jamii wakipitia Taarifa za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto iliyowasilishwa na kujadiliwa kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa
Chuo Kikuu cha Dodoma na kuhitimishwa leo tarehe 1 Aprili, 2017. Taarifa hiyo
ambayo imepitishwa na Kamati kwa maandalizi ya vikao vya Bunge la Bajeti la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
linalotarajiwa kuanza mapema mwezi Aprili, 2017. Wengine katika mstari wa nyuma
ni Wakurugenzi waandamizi wa Wizara hiyo. Kikao hicho cha siku mbili kilianza
Alhamis tarehe 31 Machi na kuhitimishwa tarehe 1 Aprili, 2017 katika ukumbi wa
Chuo Kikuu cha Dodoma.
Baadhi ya waheshimiwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya
Jamii Taarifa za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto wakipitia
maelezo ya Taarifa iliyowasilishwa na kujiaandaa kwa ajili ya majadiliano wakati
wa kikao cha siku mbili kilichofanyiaka ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na
kuhitimishwa leo tarehe 1 Aprili, 2017. Taarifa hiyo imepitishwa na Kamati kwa
hatua za maandalizi ya vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajiwa kuanza mapema
mwezi Aprili, 2017. Wengine katika mstari wa nyuma ni Wakurugenzi waandamizi wa
Wizara. Kikao hicho kilianza Alhamis tarehe 31 Machi na kuhitimishwa tarehe 1
Aprli, 2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.







0 Comments