Mwuonekano wa jengo la Mahakama ya Watoto iliyopo katika Jiji la Mbeya.
Na
Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania
Hivi
karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuhusu habari za vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa watoto.
Kutokana
na kukithiri kwa vitendo hivyo, viongozi mbalimbali wamekuwa wakitoa matamko ambayo yanaitaka jamii kufahamu haki
za mtoto ikiwa ni hatua ya kuwaepusha watoto wasiathiriwe na tabia
hatarishi.
Miongoni
mwa viongozi hayo ni Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Waziri wa
Afya,Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Mhe.
Ummy Mwalimu akiwemo Naibu wake. Dkt. Hamis Kingwallah na baadhi ya
viongozi wengine mbalimbali.
Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa asasi za kiraia na dini mbalimbali wameungana ili kuhakikisha watoto
hao, wanakua katika maadili mema na kuweza kutimiza ndoto zao.
Mbali
na hilo, kuhakikisha kwamba watu
wanaowarubuni watoto wanachukuliwa hatua za kisheria.
Mahakama ya Tanzania
kupitia Mpango Mkakati wa Miaka
Mitano yaani 2015/16 hadi 2019/20, imejenga
Mahakama nyingine ya
watoto ambayo iko katika Jiji la Mbeya.
Kupitia mpango huo, hivi
sasa Tanzania ina mahakama mbili za watoto ambazo moja iko katika jiji
la Dares Salaam na nyingine jiji la
Mbeya.
Mahakama
hizi mbili ziko katika maeneo ya
katikati ya jiji, ikiwa dhamira ya Mahakama ya Tanzania, kuhakikisha kwamba inaboresha huduma
za utoaji haki na
kusongeza huduma zake karibu
na wananchi.
Mahakama
ya Watoto ni Mahakama ambayo imeanzishwa kisheria kwa lengo la kushughulikia
kesi maalum zinazohusu watoto.
Umri
ambao Mahakama hiyo mtoto ni mtu aliye na umri wa chini ya 18 kama Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyosema sura ya kwanza,
kifungu cha 5.-(1) na ilivyo katika Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 pamoja na kanuni zake,
marekebisho ya mwaka 2006.
Mahakama
hii inashughulikia makosa mbalimbali ambayo yanaweza kufanywa na watoto kama shuleni, mitaani na sehemu nyinginezo.
Kuna
mambo
mbalimbali ambayo pia Mahakama hii inayashughulikia mfano vile taratibu za kuasili watoto na
mambo ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na mchakato mzima wa kufanya hivyo,
ikiwemo kupokea mashauri ya madai.
Usikilizaji
wa mashauri katika Mahakama hii,
hufanyika faragha. Lengo la usikilizaji wa mashauri haya kusikilizwa kwa siri ni kulinda maslahi ya mtoto.
Hivyo jamii
inapaswa kuzifahamu haki
za mtoto kama vile haki ya kuishi, kupata huduma bora za afya,
mahali pa kuishi.kupata elimu, haki ya kutambuliwa, haki ya kurithi mali, haki
ya kutonyanyaswa, ikiwemo kutofanyiwa vitendo
vya ukatili wa kijinsia.
Kwa
mujibu wa taarifa
ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Sihaba Nkinga, akizungumza
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Ukeketaji,iliyofanyika
Desemba 5, mwaka jana, Sihaba Nkinga, alisema hali bado ni
mbaya.
Katibu
Mkuu huyo alifafanua kwamba taarifa zinaonyesha kuwa mtoto mmoja kati ya watatu
wa kike na mtoto mmoja wa kati ya saba wa kiume walifanyiwa ukatili wa kingono.
Kupitia
maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya
Pangani, mkoani Tanga, Bi Zainabu Issa ametaka jamii ipige vita vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto, ili kuwawezesha kufikia ndoto zao ikiwa ni hatua ya
kuwawezesha ustawi wa maisha yao na
hatimaye kulijenga taifa la kesho.
“Ninasema
kesi dhidi ya ukatili wa watoto sasa zisizidi miezi sita au mwaka, kesi zisikae,
muda mrefu Mahakamani.Ninasema sasa mtu akipatikana na hatia ya kuumpa ujauzito
mwanafunzi au kubaka afungwe miaka 30 jela,” alisema Mkuu huyo wa wilaya wakati
siku ya maadhimisho hayo yaliyofanyika Mkoani Tanga, wilaya ya Pangani.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Appi akizungumza maadhimisho hayo
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, alipiga marufuku vitendo vya baadhi ya
walimu kuwafungia mageti wanafunzi wanapochelewa kufika mashuleni kwa kuwa
vinaweza kuwasababishia watoto kujiunga na makundi yenye tabia hatarishi.
Alisema
ili kuweza kuwaepusha
watoto kutoathiriwa na tabia
hatarishi, Mkuu huyo alipendekeza walimu
watumie adhabu mbadala pale baadhi ya wanafunzi
wanapofanya makosa wakiwa mashuleni.
Alisema
adhabu mbadala zinaweza kutolewa na
walimu, wakati wa kipindi
cha mapunziko.
Hakimu
Mkuu wa Mahakama ya Mwanzo Mjini
Mbeya, Mhe. Onesmo Zunda
akizungumzia kuhusu uzoefu wa
usikilizaji kesi za watoto zinazohusiana na madai alisema amekuwa akisikiliza kesi za ndoa na talaka nyingi
kutoka
vijijini kuliko mjini.
“Kuna
changamoto katika kusikiliza kesi hizi. Miongoni mwa changamoto
tunazokabiliana hizo ni mgawanyo wa mali
hasa pale inapotoa mtu anapokuwa amefariki dunia au wazazi kutengana mmojawapo akiwa ana fedha au mali au kaoa mke mwingine. Nyingi hivyo
mgawanyo wa mali huwa
unaleta malalamiko katika baadhi ya familia,” alisema Mhe. Zunda.
Alifafanua
kwamba katika kesi hizo ni Baba anapotaka kubaki na watoto
halafu mama hataki. Hata hivyo
anasema Mara nyingi mama
huwa anataka kubakia na watoto, lakini baba
hataki kutokana na tabia ya mama.
“Hivyo
tunatumia sheria pale ndoa inapotaka kuvunjika tunachoangalia zaidi ni maslahi ya mtoto hata kama mtoto ana umri wa zaidi ya miaka 7,” anasititiza Mhe. Zunda.
Akitolea mfano wa kesi mojawapo, ambapo alisema alitoa
maamuzi kwamba mtoto
abaki kwa baba kwa sababu mama alikuwa na tabia
ya ulevi. Alisema uamuzi huo kwa mujibu wa shuhuda za watoto.
Ingawa kulingana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ni jukumu la baba kuwapa watoto
matunzo japo jukumu la kuwalea watoto
ni la wazazi wote. Hatahivyo, mwanamke
anatakiwa achangie katika kuhudumia watoto. Iwapo wazazi wametengana amri ya matunzo hutolewa na Mahakama ili baba asiyeishi na mtoto.
Matunzo hayo
huwa ni pamoja na kutoa
nguo, chakula, kugharamia masomo shuleni na matunzo yataendelea hadi
kufikia umri wa miaka 18.
“Licha ya changamoto tunazozipitia tunajitahidi
kuzitatua kwa kutumia sheria ,hakuna
rufaa zinazofunguliwa,”alisema Mhe. Zunda.
Mhe. Zunda
alizitaja takwimu za kesi za
ndoa na talaka walizozipokea kwa kipindi cha mwaka huu yaani Januari hadi Machi 23,mwaka huu, kuwa 26 na hivyo kati ya hizo 11 bado zinaendelea kushughulikiwa na nyingine
zinaendelea kufanyiwa kazi.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mwanjelwa,
Mhe. Happiness Chuwa, alisema ili
kukabiliana na tatizo la kesi zinazo husiana na watoto ni vema jamii ikiwa ina tabia
ya kuwatambulisha watoto na kuandika wosia.
Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto, iliyopo eneo
la Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Devotha Kissoka, akizungumza wakati wa Wiki ya Sheria
iliyofanyika mwaka huu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam,
alisema mtoto akikosa anaweza kupelekwa katika
makao ya watoto.
Ikiwa
kuna tatizo, ambalo limeleta mabishano kuhusu mtoto baba yake au wazazi wake ni wakina nani?
Mahakama hiyo inatoa amri Mkemia Mkuu wa
Serikali kufanya vipimo vya utambuzi (DNA testing).
Alizitaja takwimu zinazohusu kesi za madai katika
Mahakama hiyo za kipindi cha mwaka
2016 ni 154 na katika kipindi cha mwaka 2015 zilikuwa kesi 19.
Hakimu
huyo alifafanua kwamba sababu ya kuongezeka kwa kesi hizo ni hali ya uchumi,
hivyo hali hiyo imetokea kwa watoto
walio nje ya ndoa.
Alisema
Mahakama hiyo, pia huwa inasikiliza kesi
za jinai mfano wizi wa kutumia silaha, kujeruhi
na kuua.
Mhe. Kissoka
aliongeza kwamba ieleweke kwa mujibu wa Sheria, mtoto aliyechini ya umri
wa miaka kumi hawezi kutenda kosa la jinai.
Desemba
5, mwaka huu Tanzania iliazimisha Maadhimsho ya Kupiga Vitendo vya Ukatili
dhidi ya Watoto, mfano kufanyishwa kazi ngumu, kubaka na kuolewa chini ya umri
mdogo, au kutopewa fursa ya kupata elimu bora kwa ajili ya maisha yao ya
baadae.
Mtoto
ana haki ya kupata dhamana katika
mashitaka yote isipokuwa yale, ambayo sheria imemtaka hayana
dhamana.
Mhe.
Kisoka alizitaja adhabu ambazo hutolewa kwa mtoto, miongoni
mwa adhabu hizo ni kuachiwa kwa masharti kwa kipindi fulani, lakini kisizidi
miaka mitatu, adhabu ya kulipa faini, adhabu
ya kuripoti kwa Afisa Ustawi wa
Jamii, adhabu ya kupelekwa katika shule maalum.
Pamoja
na adhabu hizo mahakama ina uwezo wa kutoa amri mbalimbali kama vile kulipa
faini, kuachiwa bila masharti yoyote.
Kutokana na maoni ya watu mbalimbali mfumo mmoja wa kisheria na nguvu za pamoja zitasaidia kupunguza au
kutokomeza vitendo vya kikatili na unyanyasaji
dhidi ya watoto.
Hii inatokana na sababu bado umri wa mtoto bado
ni tatizo kwa kuwa mtoto ana weza kuolewa
akiwa na umri wa miaka 14 au kuoa
wakati huohuo mtu anaitwa mtoto
akiwa na umri chini ya miaka 18.

0 Comments