Kumekuwa
Na Mkanganyiko Wa Habari Na Upotoshwaji Wa Taarifa, Ambazo Si Sahihi Kuhusiana
Na Yanga Kuchezesha
Kikosi
Cha Pili Hapo Jana Dhidi Ya Kombaini Ya Majeshi Katika Uwanja Wa Jamhuri Mjini
Dodoma.
Naomba
Kuliweka Jambo Hili Wazi Na Kuondoa Sintofahamu Zisizo Na Msingi Na Pengine
Kufunga Mjadala Huu Rasmi.
Week
End Ya Tarehe 22 Na 23 ,Na Ya 28 Hadi 30 Tff Walitupa Ratiba Ambayo Inaonyesha
Hakuna Mchezo Wowote Local League,
Au
Fa Cup.Na Ratiba Yetu Ilionyesha Tutacheza Tarehe 22 Fa Cup Dhidi Ya Prisons Tu
Kwa Kuwa Ni Kiporo,Na Ukiangalia Ni Wiki Ya Pili Sasa Ligi Haichezwi Kutokana
Na Ratiba Ya Chan Yaani Mashindano Ya Kimataifa Ya Caf Kwa Timu Za Taifa Kwa
Wachezaji Wa Ndani.
2.Baada
Ya Kupata Ratiba Ya Mapumziko Ya Wiki Mbili Bila Michezo Ya Ushindani ,Kama
Viongozi Tukaona Si Busara Wachezaji Wakae Bila Michezo Ya Kujipima Nguvu Ili
Kuendelea Kujijenga Kuwa Katika Ushindani Muda Wote.
Tukaona
Wiki Mbili Ni Nyingi Mno Bora Tupate Michezo Ya Kujipima Nguvu Yaani Friends
Matches Katika Majuma Haya Mawili.
Tulipokea
Barua Kutoka Arusha Tucheze Mechi Mbili Tarehe 29 Na 30 Dhidi Ya Madini
Na Afc,Tukakubaliana Nao Pia Tutaenda Huko.
Tukapokea
Barua Ya Dodoma Tucheze Tarehe 26 Tukakubali Pia.
Sasa
Tatizo Limekuja Kwa Tff Kufanya Droo Tarehe 23 ,Na Kututaka Tucheze Tarehe 30
Nusu Fainali Ya Fa Cup Ratiba Ambayo Haikuwepo Kabla Ya Hapo ,Sisi Tulikubali
Kucheza Michezo Hiyo Tukijua Hakuna Mashindano Yoyote Ndani Ya Tarehe Hizo.
3.Nakiri
Kabisa Kuwa Tatizo Limesababishwa Na Ratiba Zisizoeleweka Za Tff Tusingefika
Hapo,
Kama
Ratiba Ya Tff Ingekuwa Si Kukurupuka Tusingefika Hapo Leo.
Tumecheza
Mechi Ya Kiporo Na Prisons Tukashinda Huku Tukiwa Na Majeruhi Wanane Key
Players.
Vicent
Bossou
Donald
Ngoma
Haruna
Niyonzima
Juma
Abdul
Malimi
Busungu
Ally
Mustapha
Anthony
Mateo
Deus
Kaseke
Siku
Ya Pili Ratiba Inatoka Tucheze Nusu Fainali,Narudia Tena Nusu Fainali Tucheze
Ndani Ya Siku Saba.
Kwa
Vyovyote Vile Hata Ingekuwa Vipi ,Kwa Kikosi Tegemezi Cha Wachezaji 18
Tu,Kukichu Kua Na Kwenda Kukipiganisha Katika Michezo Miwili Mfululizo Ambao
Mmoja Hauna Tija Kabisa Tena Michezo Hiyo Ipishane Kwa Siku Tatu Tu, Hii
Haijawahi Fanywa Na Timu Yoyote Duniani.
4.Kwa
Kuliona Hilo Na Kwa Mapenzi Ya Dhati Kabisa Kutoka Mioyoni Mwetu Viongozi Dhidi
Ya Wapenda Mpira Wote Wa Mkoa Wa Dodoma Na Maeneo Ya Jirani,Viongozi Kwa Pamoja
Sote Tulitafakari Tukasema Kheri Ya Nusu Shari Kuliko Shari Yenyewe.
Kwa
Pamoja Tukahamua Kupeleka Timu Ya Kikosi Cha Pili Wakichanganyika Na Wale Wa
Kikosi Cha Kwanza Ambao Hawajatumika Muda Mrefu Waungane Na Vijana Hao Kwenda
Kuwapa Burudani Wananchi Wa Kanda Ya Kati Dodoma.
5.
Nashukuru Timu Ikiongozwa Na Mimi Mjumbe Mkemi,Mjumbe Hashimu Na Mjumbe
Siza Imefika Salama Na Bado Ipo Salama Salmin Na Jana Imeonyesha Kiwango Cha
Juu Kabisa Na Wale Waliokuwa Hawaamini Waliacha Viti Vyao Na Kushangilia Soka
Safi Na Maridadi La Vijana Wa Yanga.
Mpaka
Nikawatania Vijana Ni Hali Hii Wangekuja Baba Zao Ndiyo Msingekaa Vitini Muda
Wote.
Kwa
Machache Ni Hayo Ila Na Peleka Pongezi Kwa Benchi La Ufundi La Yanga B Chini Ya
Kocha Shadrack Msajigwa Kwa Kiwango Bora Kabisa Cha Timu Yake Amewapika Vizuri
Hakika Hiki Ni Kikosi Hadhina Maridhawa Ya Yanga Hapo Baadae.
Nitakuwa
Mchoyo Wa Fadhila Kwa Pato Ngonyani Alikuwa Captain Jana Kiwango Kizuri Hakika
Anarudi Sasa.
Yote
Katika Mwisho Pongezi Kubwa, Nzuri Sifa Kedekedee Kwa Yusuf Mhilu Mfungaji Bao
La Kusawazisha Dhidi Ya Majeshi,Siyo Sifa Hizi Kwa Ajili Ya Goli Tu La Hasha
Hakuna Aliyekaa Bila Kutoa Yowe La Furaha Kila Aliposhika Mpira, Huyu Ni Messi
Wa Tanzania Kwa Vizazi Vipya Vya Mpira Tanzania.
Mwisho
Kabisa Naliomba Shirikisho La Mpira Tanzania (TFF), liwe Linatoa Kalenda Au
Ratiba Ambazo Baadae Hazitaleta Mitafaruku Kama Hii Hapo Baadae .
Yanga
Oyeee
Daima
Mbele
Nyuma
Mwiko
Salum
Mkemi
Mjumbe
Kamati Ya Utendaji Yanga.
Msimamizi
Mkuu Wa Idara Ya Habari Na Mawasiliano Yanga.

0 Comments