Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili kwenye ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya
kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine,
wilayani Monduli.
Msaidizi wa Askofu,
jimbo kuu Katoliki Arusha, Prosper Lyimo akiweka shada la maua kwenye
kaburi la Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa
ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita,
iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine wilayani Monduli.
Wake za marehemu wakiwa wanaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine,
wilayani Monduli.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akiwa anaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine,
wilayani Monduli ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita,
iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
Mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson Ghulila akiwa anaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine,
wilayani Monduli katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita,
iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
Msaidizi
wa Askofu, Prosper Lyimo akihubiri wakati wa ibada ya kuadhimisha miaka
33 ya kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Sokoine
Binti wa Sokoine, Namelok na Kaka yake, Balozi Joseph Sokoine wakiwa na
wageni wengine walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya baba yao wilayani
Monduli.
Wajukuu wa Hayati Edward Sokoine wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita,
iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
Baadhi ya wageni kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria misa ya kumbukumbuku ya Sokoine.
Baadhi ya viongozi walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 33 ya
Sokoine, kutoka kushoto ni Askofu wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Mkoani Arusha, Solomon Masagwa, Mwakilishi wa Shehe Mkuu,
Rajab Kiungiza, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na
Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe kwenye picha ya pamoja
Wanakwaya wakiandamana kuelekea eneo la ibada tayari kwa Misa Maalum.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka akibadilishana mawazo na
mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson
Ghulila pamoja aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Balozi Daniel Ole
Njoolay
Mtoto wa Hayati Sokoine, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na wageni waalikwa katika misa maalum ya kumuenzi baba yake.














0 Comments