Balozi wa DStv na Mshiriki pekee kutoka Tanzania aliyeshiriki mashindano ya London Marathon yaliyofanyika leo jijini London ameibuka mshindi wa tano huku akivunja rekodi yake kwa kutumia muda wa 2:09.10 ambao ndio muda wake bora zaidi tangu aanze kushiriki mashindano ya kimataifa. Kabla ya hapo rekodi yake ilikuwa muda wa 2:09.21 aliyoiweka mwaka jana kwenye mashindano ya Lake Biwa Marathon nchini Japan.
Simbu ambaye ni
mshindi wa medali ya dhahabu wa Mumbai Marathon ameonyesha umahiri mkubwa
katika mashindano hayo hasa ikizingatiwa kuwa mashindano hayo yalikuwa
yanashirikisha vinara wengi wa riadha ulimwenguni wakiwemo Muethiopia Kenenisa
Bekele wakenya Daniel Wanjiru, Bedan Karoki na Abel Kirui.
Mara baada ya ushindi
huo salamu za pongezi zimekuwa zikimiminika huku mkurugenzi Mtendaji wa
Multichoice Tanzania Maharage Chande akisema kuwa kampuni yake imeridhishwa
sana na ufanisi aliouonyesha katika mashindano hayo.
Amesema uwekezaji
uliofanywa na kampuni hiyo katika kumdhamini Simbu umezaa matunda kwani kiwango
cha mwanariadha huyo kimekuwa kikiimarika siku hadi siku.
“Tumefurahishwa sana
na kiwango alichoonyesha Simbu kwenye London Marathon.
Hii ni ishara nzuri sana
na tunaamini atafanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya riadha ya Dunia
yatakayofanyika jijini London mnamo mwezi Agosti mwaka huu”
Kwa upande wake,
meneja wa mwanariadha huyo Francis John amesema kuwa ameridhishwa na kiwango
alichoonyesha Simbu na kwamba punde tu atakaporejea wataanza maandalizi kwa
ajili ya ushiriki wake katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika mwezi agost
mwaka huu.
Katika mashindano hayo
nafasi ya kwanza imechukuliwa na Mkenya Danie Wanjiru (2:05:48) akifuatiwa kwa
karibu na Kenenisa Bekele (2:05:57) na Bedan Karoki (2:05:41)

0 Comments