Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya
NMB, Bw. Stephen Adili (kushoto) akitoa maelezo namna benki hiyo
inavyowakumbuka vijana katika bidhaa zao mbalimbali kwa wageni waalikwa,
Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (wa kwanza kulia) na
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) walipotembelea banda
hilo kwenye uzinduzi wa mjadala kujadili changamoto mbalimbali na
kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha.
Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (kushoto) akimkabidhi
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya
NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) cheti kilichotolewa na UN-CDF Tanzania,
kwa NMB kwenye kampeni kuwahamasisha vijana kupata uelewa wa masuala ya
fedha wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kujua huduma anuai
zinazotolewa na benki hiyo na kuwagusa vijana. NMB imeshiriki
kufanikisha kampeni hizo.
Baadhi ya wageni waalikwa katika kongamano la kampeni zilizowakutanisha
vijana kujadili changamoto mbalimbali, wakipokea vipeperushi ndani ya
banda la NMB kwenye kongamano hilo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akizungumza na vijana katika
kampeni zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali,
ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya
fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.
Baadhi ya wageni waalikwa na vijana wakiwa katika kongamano la kampeni
zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja
na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala ya fedha.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya
NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) akifurahia cheti kilichotolewa na
Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (kushoto) kwenye
kampeni kuwahamasisha vijana kupata uelewa wa masuala ya fedha wakiwa
ndani ya banda la Benki ya NMB kujua huduma anuai zinazotolewa na benki
hiyo na kuwagusa vijana.
Nikki Wa Pili (kushoto) akizungumza na vijana walioshiriki kampeni
zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja
na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na
kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.
- Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana, Eliakimu Mtawa (kushoto) akizungumza na vijana walioshiriki kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.
- Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) akizungumza na vijana katika kampeni zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazowainua vijana kimitaji.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya
NMB imeshiriki kampeni zilizoendeshwa na Shirika la Kimataifa la Mfuko
wa Mtaji wa Maendeleo UN- CDF zinazowakutanisha vijana pamoja na
mashirika mbalimbali yanayofanya kazi kuwahusisha maendeleo ya vijana.
Kampeni hizo 'BankTheYouth' zilizowakutanisha vijana na kujadili
changamoto mbalimbali zinazowakabili zimelenga kuhamasisha vijana nchini
kupata uelewa wa masuala ya fedha pamoja na kuwaunganisha na taasisi
zinazowainua vijana kimitaji ili wafikie malengo yao.
Akizungumza
na vijana walioshiriki kampeni hizo, Meneja Mwandamizi Kitengo cha
Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili
alisema vijana wanapaswa kuungana katika vikundi na kuandaa maandiko ya
biashara ambayo yataivutia benki kutoa mikopo ili kuendesha biashara
zao. Alisema benki ya NMB imekuwa mstari wa bele kuibua bidhaa
mbalimbali za kibenki zinazolenga kuwainua vijana hasa elimu ya uelewa
masuala ya fedha na namna ya kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba.
Aliwashauri
vijana kutembelea matawi mbalimbali ya NMB na kujenga urafiki kwa
kufungua akaunti na kujiwekea akiba kabla ya kuanza kunufaika na bidhaa
mbalimbali zilizoanzishwa kuwasaidia vijana kimitaji. "...Ili benki
ikuamini lazima ujenge mahusiano mazuri, ujenge urafiki na hii ni pamoja
na kuwa na akaunti na sisi. Hatuwezi kukuamini kama hata hauna akaunti
na sisi, anza kwa kujenga mahusiano mazuri kwanza nasi ndipo
tukuamini...hatuwezi kukukopesha kama haupo karibu na sisi," alisema
Adili.
Kwa
upande wake Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika aliwataka
vijana kushiriki vema katika kampeni hizo pamoja na kukubali kubadilika
kulingana na mazingira ya sasa na kutumia fursa zilizopo ili ziwaletee
maendeleo. Aliwataka kujadiliana na kuibua changamoto anuai ambazo
zimekuwa vikwazo katika maendeleo yao.
Alisema
lazima wajiweke katika vikundi na kufuata utaratibu mzuri utakaowekwa
na taasisi zinazosaidia vijana kuelekea katika maendeleo. Aidha
aliongeza kuwa vikundi vya vijana lazima vijulikane na kufuata utaratibu
rasmi uliowekwa ili viweze kuaminika kwa taasisi mbalimbali zikiwemo za
kifedha.
Aliwaomba wajiwekee utaratibu wa kujiwekea akiba ili waweze
kuaminika zaidi.
Naye
Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana,
Eliakimu Mtawa aliwataka vijana kujenga uaminifu wa kurejesha mikopo
pale wanapopata fursa ya kukopeshwa kwani takwimu zinaonesha fedha
nyingi zinazotolewa na Serikali kuwakopesha vijana wapate mitaji
wamekuwa hawarejeshi jambo ambalo linatishia uhai wa mifuko hiyo
kuendelea kusaidia vijana wengine.










0 Comments