Vikundi vya Jooging kutoka Dodoma vikiwa
katika mazoezi ya kukimbia kutoka Viwanja vya Nyerere Square hadi Viwanja vya
Kilimani Club Mjini Dodoma.
Vikundi vya Jooging kutoka Dodoma vikiwa
katika mazoezi ya viungo katika viwanja
vya Kilimani Club Mjini Dodoma
Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku
Bilago(kushoto) Mbunge wa Kiwani (Zanzibar) Mhe. Abdalla Haji Ali (kulia)
wakifanya mazoezi ya viungo katika katika viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma ikiwa
ni kuunga mkono wito wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu
Hassan wa kufanya mazoezi.
Mratibu wa Michezo Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Salum Mkuya akizungumza
navikundi vua Jogging Club wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Viwanja vya
Kilimani Club Mjini Dodoma.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini
Daniel Shija akizungumza na vikundi vua Jogging Dodoma na kuwahakikishia Ulinzi
na usalama katika mazoezi yao.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Ofisi
ya Rais TAMISEMI na baadhi ya wabunge wameongoza vikundi vya Jogging Mkoani Dodoma
kufanya mazoezi kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Sluhu Hassan wa kufanya mazoezi.
Akizungumza
baada ya mazoezi hayo Afisa Tawala
kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Rose Lugendo amewaomba wakazi wa Dodoma
wajitokeze kwa wingi kufanya mazoezi kwa afya zao na kuimarisha mahusiano baina
yao.
“Napenda
kuwashauri wakazi wa Dodoma kujiunga na Jogging Clubs na kuwa na Utamaduni wa
kufanya mazoezi kwa Afya zao” alisisitiza Bibi Rose.
Kwa
upande wake Mbunge Wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde amewaasa vijana kujitokeza
kufanya mazoezi kila siku na sio kusubiri kufanya mazoezi mara moja kwa mwezi
kwasababu mazoezi ni sehemu ya maisha.
“Vijana
tumieni fursa hii kufanya mazoezi na kujenga afya zenu mazoezi yawe sehemu ya
maisha yenu” alisisitiza Mhe. Lusinde.
Naye
Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago amevipongeza vikundi vya Jogging Dodoma
kwa kuleta mwamko wa mazoezi katika mkoa wao na kujenga desturi ya watu kupenda
mazoezi na michezo.
Aidha
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini Daniel Shija amewahakikishia ulinzi wanamazoezi
na michezo kwa ujumla katika sehemu mbalimblai ambazo watakuwa wanafanya
michezo.













0 Comments