Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza na wadau wa afya,wataalam wa afya,na watendaji mbalimbali katika mkutano uliokuwa ukizungumzia utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi
Wadau na wataalamu mbalimbali wa afya mkoani Pwani wakifuatilia jambo kwenye mkutano uliokuwa ukizungumzia utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi.
Mratibu wa TACAIDS Pwani na kaimu Dar es salaam Charles Kamugisha akizungumza jambo kwa waandishi wa habari.
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MWENYEKITI wa kamati ya
ulinzi na usalama mkoani Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo, amewahakikishia
wananchi kuwa hali ya usalama wilaya ya Kibiti na Rufiji ipo shwari .
Aidha amesema jeshi la
polisi linaendelea na oparesheni mbalimbali za kuwasaka wahalifu wanaochafua
mkoa na taifa.
Aliyasema hayo, kufuatia
habari zinazoendelea kusemwa na kuandikwa katika baadhi ya vyombo vya habari
kuhusu mambo yanayoendelea kwenye wilaya hizo.
Mhandisi Ndikilo,aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi waliopo kwenye oparesheni hiyo na kuacha
kukimbia miji yao kama wanajiamini sio wahalifu.
"Kumekua na taarifa
zinazoendelea kuandikwa suala ambalo mkoa haujawahi kutoa taarifa zaidi ya
tukio la mauaji ya vifo nane iliyotokea april 13 na kukemea usafiri wa pikipiki
ifikapo saa 12 jioni " alisema.
Alibainisha kwamba, endapo
kutakuwa na tukio ama jambo litakalojitokeza serikali ya mkoa, wilaya, jeshi la
polisi litatolea ufafanuzi.
Mwenyekiti huyo wa kamati
ya ulinzi na usalama ambae pia ni mkuu wa mkoa huo, alieleza, kwa sasa vyombo
vya dola vinawasaka watu waliojihusisha na mauaji ya wenyeviti wa vijiji,
vitongoji na polisi .
"Jeshi la polisi ama
serikali haiwezi kumwonea mtu yoyote kwani inafanywa kwa kuzingatia
sheria"alisema.
Mhandisi Ndikilo alisema
jeshi la polisi linafanya
kazi yake kwa weledi na kazi yake kubwa ni kulinda amani ya wananchi na mali
zao.
“Nawaombeni wananchi msiwe
na hofu juu ya operesheni hiyo na hakuna haja ya kukimbia makazi yao kwani kuna
taarifa kuwa kuna watu wamehama kwenye nyumba zao na kukimbia,” alisema
Ndikilo.
Alisema kuwa watu
wanaokimbia wanatia mashaka, hawana sababu ya kukimbia nyumba zao na familia
zao kwani wanaotafutwa ni wahalifu na si raia wema.
Mhandisi Ndikilo,
alisema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili viweze
kufanya kazi zake ipasavyo.
Aliwatoa hofu watu wote
wanaofanya shughuli zao kwenye wilaya hizo kutokuwa na wasiwasi kwani ulinzi
umeimarishwa .



0 Comments