Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye
ulemavu Antony Mavunde(katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC baada ya kuzindua rasmi duka
jipya la VodacomTanzania Plc lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye
ulemavu Antony Mavunde(katikati)akikata utepe kuashiria Uzinduzi rasmi
wa duka jipya la VodacomTanzania Plc lililopo eneo la Kizota mjini
Dodoma ,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo
,Jacqueline Maturu na kushoto ni Mkuu wa maduka ya rejareja na mauzo wa
kampuni hiyo, Brigita Stephen.
Naibu
Waziri wa Kazi Vijana na Ajira,Mh.Antony Mavunde, ameipongeza kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc kwa kuzidi kuimarisha huduma zake
mkoani Dodoma hususani kipindi hiki ambacho Serikali imehamishia makao
yake mkoani humo na ofisi nyingi za serikali zikiwa zinazidi kuhamia.
Akizindua
duka jipya na la kisasa la kampuni hiyo eneo la Kizota mwishoni mwa
wiki,Mh.Mavunde alisema kuwa serikali inatambua kuwa sekta ya
mawasiliano inachochea maendeleo ya nchi haraka ndio maana imekuwa
ikifanya jitihada za kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta hii
ili kuwezesha wawekezaji kusambaza huduma za mawasiliano nchini
kote,maeneo ya mijini na vijijini.
Mkuu wa maduka ya rejareja na mauzo wa Vodacom Tanzania PLC ,Brigita
Stephen na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Jacqueline
Maturu wakimshuhudia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana
na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akikata keki kuashiria
Uzinduzi rasmi wa duka jipya la kampuni hiyo mwishoni mwa wiki lililopo
eneo la Kizota mjini Dodoma.
“Nawapongeza
Vodacom kwa kuongeza nguvu ya huduma zenu kwa kufungua duka jipya mbali
na maduka yaliyopo,hatua hii inadhihirisha kuwa mnaenda sambamba na kasi
ya serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambapo tayari shughuli
nyingi za serikali zinafanyika mjini hapa na idadi ya wakazi inaongezeka
hivyo mawasiliano bora yanatakiwa.”Alisema
Aliwataka
wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kama
vile kutembelea duka hili jipya la Vodacom kwa aili ya kupata huduma za
mawasilaino ikiwemo kujua huduma za kubadilisha maisha ya wananchi
zinazotolewa na kampuni ya Vodacom bila kusahau kujitokeza kununua hisa
zake katika mchakato wa kuuza hisa unaoendelea.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu
Antony Mavunde katikati akigongesha glasi wenye mvinyo ikiwa ni ishara
ya Uzinduzi wa duka jipya la kisasa eneo la kizota mjini Dodoma.
Kwa
upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni
hiyo, Jacquiline Materu,alisema Vodacom itaendelea kutekeleza dhamira
yake ya kurahisisha mawasiliano na kufanya ubunifu wa kiteknlojia
kupitia mtandao wake lengo kubwa likiwa ni kuwapeleka watanzania katika
ulimwengu wa kidijitali.
“Tutaendelea
kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya
mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko mengi kwenye maisha ya
watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Vodacom imejikita kwenye kupanua
wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza
kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye
uhakika”.Materu
Kampuni ya Vodacom
ambayo ni ya kwanza kuanza mchakato wa kuuza hisa zake katika sekta ya
mawasiliano nchini imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano
kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii,
hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu
kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa,
kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze
kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.





0 Comments