Mwanasheria
Rachel Kilasi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , akifafanua
sheria ya Ardhi na. 4 ya mwaka 1999 sambamba na Umiliki wa Ardhi (Haki, Wajibu
na uzingatiaji wa ulipaji wa Pango la Kodi ya Ardhi kwa Mmiliki.
......
Mwananchi
yoyote ana haki ya kupatiwa Hatimiliki ambayo ni nyaraka halali ya umiliki wa
ardhi baada ya kupata ridhaa ya Kamishna au Kamati na kulipa ada stahili.
Hatimiliki hutolewa ndani ya siku 90 mpaka 180 baada ya ridhaa husika.
Katika
fungu la 32 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, masharti ya umiliki wa
ardhi yanaainishwa kuwa ni ya aina tatu, ambayo ni; Umiliki wa miaka 33,
umiliki wa miaka 66 na umiliki ulio mkubwa zaidi ni wa miaka 99.
Aidha,
katika fungu la 33 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, inaeleza sharti
la mmiliki wa ardhi katika kutoa malipo ya pango la Ardhi kwa kila mwaka wa
fedha unapoanza.
Mwananchi
hana budi kutimiza masharti ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi kwa wakati.
Mwananchi anapokiuka sharti hili; fungu la 49 – 50 la Sheria ya Ardhi ya namba
4 ya mwaka 1999 inaeleza gharama zake ni pamoja na kutozwa tozo au riba, Kupelekwa Mahakamani na
Kufutiwa umiliki wa ardhi.
Mwananchi
zingatia ulipaji wa Kodi la Pango la Ardhi, kutimiza wajibu wako, kuondoa
usumbufu na kuongeza pato la Taifa Letu.
Na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi


0 Comments