Timu za kamba za TPDC na MUHAS baada ya kumaliza mchezo wao wa marudio kwa sare
Timu ya Kuvuta Kamba ya TPDC ikijiandaa kuingiakwenye mchuano dhidi ya Hai DC.
Katika Mchuano huo uliopangwa kuchezwa tarehe 25 Aprili, 2017 majiara ya jioni katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro timu ya TPDC ililazimi kakuvuta kamba bila ya mpinzani ili kukamilishi mchezo huo kwa kadiri ya kanuni za mchezo wa kamba.
Ndugu Joram Ngalawa ambaye ndiye kapteni wa timu ya kamba amesikitishwa kwa kitendo cha wapinzani wao kutokutokea uwanjani kwakuwa walijipanga kushindana.
“Sisi tumesikitishwa kushindana na hewa kwakuwa tulitamani saana tuvutane hapa na wanaume wenzetu ili tupimane ubavu kwa hiyo ushindi huu tumeupokea kwakuwa umetupa fursa ya kwenda mbele zaidi katika mashindano haya” alieleza kapteni wa timu.
Katika mchezo uliotangulia wa marudiano dhidi ya TPDC na MUHAS umemalizika bila ya kupata mbabe baada ya kumalizika nguvu sawa.
Hivyo sare hiyo imeifanya TPDC kuibuka mshindi kwa pointi moja kutokana na ushindi wa TPDC katika mzunguko wa kwanza.



0 Comments