Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imetoa jarida lake la mwaka (Toleo Na. 8). Jarida hili
haliuzwi. Kuna nakala chache ambazo zinapatikana Wizarani katika Kitengo cha huduma
kwa mteja. Aidha, kutakuwa na nakala nyingine chache ambazo zitasambazwa katika
maeneo mbalimbali kama; Wizarani na katika Ofisi za Halmashauri nchini.
Jarida hili litapatikana pia
hivi karibuni kwenye tovuti ya Wizara (www.ardhi.go.tz).
Mwananchi pata nakala yako
upate kuhabarika kuhusu shughuli na matukio mbalimbali ya Wizara.
Na.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.


0 Comments