Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa tamko kuhusu Siku ya Malaria Duniani
kwa waandishi wa Habari Mjini Dodoma na
kusisitiza kuwa vipimo vya Malaria na Dawa za Mseto ni bure kwa vituo vyote vya
Afya vya Umma nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua Kitabu cha Mapambano
dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka
kamouni ya Gullin Pharma mara baada ya kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya
Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.
Picha zote na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO.
.........
Na
Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema
kuwa Serikali haitosita kuwachukulia hatua mtumishi yoyote katika vituo vya
Afya vya Umma nchini watakaobanika kutoza fedha katika kutoa huduma ya vipimo
vya malaria na kuuza dawa za Mseto kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.
Ameyasema
hayo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutoa tamko la Siku
ya Malaria Duniani na kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kupata huduma ya kupima
malaria pamoja na dawa za kutibu malaria bure katika vituo vya Afya vya Umma.
“Huduma
ya kupima Malaria na dawa za Mseto zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vyote
vya Umma vya Huduma za Afya nchini na hatutosita kuwachukulia hatua watakaokiuka
kutekeleza agizo hili.Alisistiza Mhe. Ummy.
Aidha
amwewaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza agizo hilo na
kulisimamia kwa karibu ili kuondoa usufumbu kwa wananchi wanapotaka kupatiwa
huduma hiyo.
Mhe
Ummy Mwalimu amewashukuru wadau wote waliochangia kwa hali na mali katika mafanikio
yaliyofikiwa ya mapambano ya dhidi ya Malaria nchini.
Siku
ya Malaria Duniani uadhimishwa kila Aprili 25 ya kila mwaka na kwa mwaka huu
kauli mbiu ni “ Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii”.



0 Comments