Meneja Masoko wa TV 1 Tanzania , Gllian Rugumamu akizungumza
na waandishi wa habari juu ya mpango wa T V 1 Kusaidia timu hiyo hili
iweze kusafiri kwenda Italy kushiriki mashindano ya Dunia.
Katibu mkuu wa Chama cha Tennisi nchini , Irene Jackson
Mwasanga akizungumza na waandsihi wa habari juu ya mpango wa kuiwezesha
timu ya mchezo wa Tennisi kwa walemavu.
mcheza Tennisi akiwa katika mazoezi ya kawaida katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam leo.
Mcheza Tenisi Vosta Piter akijaribu kurudisha mpira
uliopigwa na mwenzie katika mazoezi ya mchezo huo katika Viwanja vya
Gymkhana Dar es Salaam.
Timu ya Magongo ya Tennis inahitaji milioni 120 ili
kuweza kushiriki mashindano ya kimataifa yanayotarajia kutimua vumbi Mei
1 hadi Mei 6 nchini Italy.
Akizungumza
na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Rais wa timu hiyo, Denis
Makoi amesema kuwa hadi sasa wamepata dola 3500 ambazo dola 3000
zimetolewa na Kampuni ya TPS na dola 1500 zimetolewa na shirikisho la
Tenis la Kimataifa.
Amesema mashindano
hayo ni mhimu kwa timu hiyo kwani wao ndio mabingwa wa Afrika hivyo
kushiriki kwao kutaongeza kuwa na uwezo na kuiletea Taifa heshima ya
mchezo huo.
Makoi amesema kuwa TV One
wamejitoa kuungana na katika kutafuta fedha hizo ili timu hiyo iweze
kushiriki mashindano hayo yatayoifanya Tanzania kuingia katika ramani
mchezo wa Tenis.
Meneja wa Masoko wa TV
1, Gillian Rugumamu amesema wamejitoa katika kuhamasisha watanzania
kuchangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo.
Gillian amesema kama chombo cha habari wanawajibu wa kuhamasisha mchezo wa tenis kutokana na vjana kuwa na uwezo wa mchezo huo.
Amewaomba
watanzania kuchangia kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa M-Pesa kwa
kuingiza namba 5590901 kwa Benki ya NIC kwa fedha ya Kitanzania A/C
No.2000021086 na dola za Kimarekani kwa akaunti A/C NO. 2000021094.

0 Comments