Na Carlos Nichombe
UONGOZI WA Klabu ya
Simba umesema hauwezi kuzungumzia kitendo cha wao kunyang’anywa pointing
tatu na Kamati ya Sheria,katiba na Hadhi za wachezaji mpaka hapo
watakapopewa nakala ya maamuzi ya kikao cha kamati hiyo.
Makamu wa Rais wa Simba,
Godfrey Nyange (Kaburu) alisema wamesikia taatifa mbalimbali zenye
mapungufu kutoka kwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
ambazo zinaonesha kutokuzingatia kanuni na taratibu katika kupokonya
pointing klabu yao.
Kaburu alisema
wanashangazwa na kitendo cha katibu MKUU wa Shirikisho la Soka
Tanzania,Selestine Mwesigwa kukiri kuwa Mchezaji wa Kagera Sugar Fakh
Mohammed alikuwaa na kadi tatu hivyo kuamua kuinyang’anya Simba pointing
kutokana na kutotimiza baadhi ya vigezo wakati wa kudai haki yao.
Alisema wanashangaa
kuona TFF inashindwa kutimiza majukuku yao wap wenyewe pasipo kusubiri
klabu ziendekupeleka malalamiko na ndipo waweze kuchukua maamuzi
wanayopaswa kuyachukua.
“Hili suala lipo wazi
kutokana na wao wenyewe kukiri kwamba yule Mchezaji anakadi tatu pasipo
kujali kama sisi tumekata rufaa au hatujakata,pia hatujajua ni mambo
gani yanayoendelea kwa sababu mpaka hivi sasa hatujapata barua rasmi
inayotueleza kile kilichofanyika kwa siku zote ambazo kamati ya
Sheria,katiba na Hadhi za wachezaji walijadili kwa siku zote,” alisema
Kaburu.
Hata hibyo Kaburu
aliongeza kuwa in vyema TFF ikatambha wajibu wake katika kuhakikishasoka
la Tanzania linazidi kuganyavizuri kadri zinavyozidi kwenda mbele kwani
kitendo cha kutoa na kinyang’anya pointing kinaharibu heshima ya soka.
Wakati huo huo,Katibu
MKUU wa YANGA,Boniface Mkwasa aliitaka TFF ku badili kanuni na taratibu
zinazoruhusu timu Fulani kupewa pointi za mezani endapo wanakuwa
wameshindwa kupata ushindi katika Michezo yao ya awali.
Alisema kitendo cha
kutoa pointi za mezani kinazidi kuzorotesha soka la Tanzania na timu
ndogo ndogo zimekuwa ndio waathirika wakubwa wa vitendo hivyo.

0 Comments