Tiganya Vincent,
RS-Tabora
27.4.2017
Wananchi wa Mkoa wa Tabora wanakwenda kuona wagonjwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete wameondokana na adha ya muda mrefu ya
kunyeshewa mvua na kukaa juani baada ya kukamilika na kuzinduliwa kwa Jengo la
Mahali pa Kungonjea kuona wagonjwa.
Jengo hilo lililojengwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora na umegharimu shilingi milioni 18 hadi kukamilika.
Uzinduzi huo umefanywa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen
Mlozi wakati wa sherehe fupi zilzofanyika katika Hospiali ya Rufaa ya Mkoa huo
Kitete.
Alisema kuwa kukamilika kwa
jengo hilo kwa muda kumesaidia kuondoa kilio cha muda mrefu cha viongozi na
wananchi cha kutaka lijengwe eneo la watu kupumuzika wakati wakisubiri muda wa
kuona wagonjwa wao wanapata matibabu katika Hosptali hiyo.
Kaimu
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliipongeza Seketarieti ya Mkoa wa Tabora
kwa kuwa wabuni hadi kufanikisha ujenzi huo kwa kiwango cha juu na
gharama nafuu.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alisema kuwa
ujenzi wa jengo hilo umefanywa kwa kutumia fedha za usimamizi wa miradi ambapo
Seketarieti ya Mkoa huo imepunguza katika fedha zake za kufuatilia miradi.
Alisema kuwa hatua hiyo imesaidia kupatikana kwa fedha hizo
zilizosaidia kukamilisha kwa jengo ambalo ambalo litasiadia kuepusha wananchi
hao na hatari za kugongwa na baiskeli au pikipiki kutokana na kukaa kando kando
ya barabara.
Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kabla ya ujenzi huo
walitaka kumtumia Mhandisi kutoka nje ambapo alidai apatiwe shilingi milioni 35
ili afanikishe ujenzi huo , lakini walipoamua kutumia mwandishi wa ndani wameokoa
kiasi cha milioni 17.
Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa
Wakurugenzi wote Watendaji wa Halmashauri nane(8) za mkoani Tabora kuhakikisha
wanajenga jengo kwa kila Hospitali la Mahali pa wananchi kuongejea kuona wagonjwa
wao.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwaondelea kero wananchi na
kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwajali wanyonge.
Aidha , Dkt. Ntara aliwaahidi wananchi kuwa baada ya kukamilika
kwa jengo hilo atajitadi kuwanunulia runinga ili wanapokuwa wanasubiri kuona
wagonjwa wafutilie taarifa mbalimbali za habari zinaendelea za ndani na nje ya
nchi.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora
wanatarajia kujenga Kliniki mbili katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete
kwa ajili ya vijana na wakinamama.
Alisema kuwa lengo la kutaka kufanya hivyo ni kutaka kutoa elimu
kwa vijana hasa mabinti kwa ajili ya kupunguza ndoa na mimba za utotoni mkoani
Tabora.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete ilijengwa katika miaka
ya 1909 lakini ilikuwa haina sehemu ya watu kukaa wakati wakisiburi kuona
wagonjwa.

0 Comments