Header Ads

WIZARA YA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO IMEPOKEA KWA MSHTUKO TAARIFA ZA KUTOWEKA KWA MWANAMUZIKI ROMA MKATOLIKI

Wizara kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki”  tangu tarehe 5 Aprili 2017.
Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai. Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.
Kutokana na hali hiyo,Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.
Imetolewa na
Zawadi Msalla       
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
07/04/2017

No comments

Powered by Blogger.